The Bournemouth Protocol on Mass Grave Protection and Investigation - Swahili translation

Page 1

Itifaki ya Bournemouth kuhusiana na

Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki

1


© 2020 Melanie Klinkner na Ellie Smith Haki zote zimehifadhiwa. ISBN: 9781858993218 Picha la jalada © 2


Utangulizi

na Malkia Noor, Kamishna wa Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea Kama Kamishna wa Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea (ICMP) tangu 2001, nimekuwa na bahati na mwenye hisia nyingi kushuhudia mabadiliko ya kihistoria kuelekea uwajibikaji wa Taifa katika kuwajibikia watu waliopotea kulingana na sheria. Katika miaka ya 1990, taasisi za haki za ndani na za kimataifa zilianza kuchunguza maelfu ya visa vya makaburi ya halaiki katika Yugoslavia ya zamani. Hii iliweka msingi wa mikakati ya msingi wa sheria ya kupata haki za manusura na kukuza imani ya umma katika uwezo na utayari wa serikali wa kudumisha uchunguzi madhubuti na wa haki wa watu waliopotea. Uchunguzi huu ulijumuisha utumiaji thabiti wa njia za kisayansi ili kupata na kutambua waliopotea. Ime kuwa dhahiri pia katika kipindi hiki kwamba uchunguzi sahihi wa visa vikubwa vya watu waliopotea, iwe ni kutokana na mgogoro, ukiukwaji wa haki za binadamu, majanga, uhalifu uliopangwa au uhamiaji, ni uwekezaji katika mshikamano wa kijamii, na urejesho kutokana na migogoro na uzuiaji, na vile vile amani endelevu na usalama wa binadamu. Wajibu wa kufanya uchunguzi madhubuti wa ukiukaji na udhalimu wa haki za binadamu uko chini ya Mataifa, bila kujali ni nani aliyefanya ukiukaji na udhalimu huo. Kushindwa kuchunguza visa vya watu waliopotea kwa njia inayofaa, ikiwa ni pamoja na hali za kutoweka, ni ukiukaji wa haki za kimsingi za binadamu za watu waliopotea na wanafamilia zao. Pia ni ukomeshaji hatari wa sheria. Uchunguzi madhubuti kwa hivyo unawakilisha kujitolea halisi na muhimu katika kushughulikia historia ya uhalifu wa zamani. Mnamo mwaka wa 2008, chapisho lililoandaliwa chini ya mwongozo wa wasomi katika Chuo Kikuu cha Bournemouth liliwasilisha mkusanyiko wa kwanza wa hali na mafunzo kutoka kwa uchunguzi wa kisayansi wa makaburi ya halaiki. Hii ilikuwa shughuli ya kushirikiana inayolenga kuunda Taratibu za Kawaida za Utekelezaji. Itifaki mpya ya Bournemouth kuhusiana na Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki inaendeleza mkakati huu wa utafiti, unaojumuisha kazi ya wataalam wa kimataifa wanaowakilisha taaluma na mashirika mbalimbali, ili kufafanua viwango kuhusiana na suala hili muhimu. Itifaki ya Bournemouth kuhusiana na Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki inategemea kwa udhabiti dhana

kuwa viwango vya uchunguzi na ulinzi zinazotumika kwa makaburi ya halaiki ni lazima viunge mkono juhudi za kuthibitisha ukweli kuhusu kile kilichotokea na kuwezesha utafutaji wa haki. Ni kupitia uchunguzi kwamba Taifa linaonyesha maana kwa dhamana za haki za binadamu. Uchunguzi wa uhalifu unaongoza mara kwa mara juhudi za kutafuta na kufukua makaburi ya halaiki kufuatia mgogoro wa vita vya silaha, ukiukaji na udhalimu wa haki za binadamu, na vitendo vingine vya uhalifu. Unalenga kupata ushahidi wa uhalifu na ni sehemu ya mradi mkubwa unaorejelewa na mahakama kama haki ya uchunguzi madhubuti. Itifaki ya Bournemouth kuhusiana na Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki ni hatua muhimu mbele katika kutoa ufafanuzi kuhusiana na kanuni na viwango vya kimataifa. Itawezesha ushirikiano mkubwa kati ya mashirika katika mipangilio mipana. Makaburi mengi ya halaiki na maeneo ambayo vurugu za kutisha na upotezaji wa binadamu zimetokea lazima zilindwa dhidi ya uingiliaji na kuchunguzwa kulingana na viwango ambavyo ni halali na vya heshima. Tunawajibikia hili kwa familia za waathiriwa, na kwa jamii kwa ujumla. Itifaki iliyowasilishwa hapa imehamasishwa na inatokana pakubwa na wahusika wengi wanaohusika katika ulinzi wa makaburi ya halaiki na michakato ya uchunguzi, kutoka kwa taaluma za kisheria, uchunguzi na za kisayansi hadi ushirikiano wa jamii na usaidizi wa familia, kila mmoja ikiwa na sheria na viwango vyake vya kazi ya kitaalam. Kwa niaba ya ICMP, inanipa furaha kubwa kuanzisha Itifaki ya Bournemouth kuhusiana na Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki.

Mtukufu Malkia Noor Kamishna wa Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea

1


Dibaji

na Dak. Agnes Callamard, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na Mauaji ya Kiholela, Yasiyo ya Haki au Yasiyo na Msingi Makaburi mengi ya halaiki sio visa vya pekee katika historia ya wanadamu. Yametawanyika kote ulimwenguni na katika kila eneo. Baadhi yake ni ya karne za nyuma, wakati mengine yamegunduliwa hivi majuzi tu. Hata hivyo yote yanatokana na visa muhimu dhahiri - ukweli ambao mara nyingi haujaelezwa, umekataliwa, kufichwa au kuzikwa. Kama Mwandishi Maalum wa UN anayezingatia haki za binadamu katika muktadha wa mauaji ya kiholela na yasiyo ya haki au yasiyo na msingi, ninajua kuwa makaburi ya halaiki yanaweza kuwa matokeo ya vita vya silaha, yanayohusiana na vitendo vya uhalifu au matokeo ya upuuzaji wa Taifa. Ninajua pia kuwa maeneo ya mauaji ya halaiki na mazishi ya halaiki ni mahali ambapo ukiukaji mwingi wa haki za binadamu unaweza ukuwa ulifanyika, labda mara kwa mara, katika kipindi cha muda. Maana ya kibinafsi, ya kidini, ya kitamaduni na ya kihistoria ya eneo la kaburi la halaiki na matukio yanayohusiana na uundaji wake hutofautiana kutoka sehemu hadi nyingine, kutoka kwa mtu binafsi hadi mwingine, kutoka jamii hadi nyingine, kutoka nchi hadi nyingine. Lakini umuhimu wake unazidi mzozano na unapita mipaka na vizazi. Inatoa jukumu la uhifadhi wa kaburi la halaiki na ukumbusho kuwa wajibu wa Vizazi vyote, vya zamani, vya sasa na vya baadaye, ili kuruhusu buriani za mwisho na kutoa heshima za mwisho. Kwa hivyo, haipaswi chini ya hali yoyote uwepo kwa kaburi la halaiki kukataliwa au kufichwa, wala eneo kuharibiwa au kuangamizwa. Haipaswi kwa hali yoyote wale wanaotafuta au kuzungumza kuhusu makaburi ya halaiki wafungwe jela, watishwe au wanyamazishwe. Badala yake, haki kamili za binadamu-mbinu ya msingi lazima ichukuliwe. Utendeaji, usimamizi na utumishi mzingativu unahitajika ambao unalinda heshima ya wafu, unapunguza mateso ya familia na jamii kadri inavyowezekana, unawezesha utafutaji wa ukweli na haki, na unaashiria kwa wote kujitolea kwa kudumu wa kutorudia tena. Itifaki ya Bournemouth kuhusiana na Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki ni mchango mkubwa kwa hatima hii. Inatoa ufafanuzi unaohitajika wa makaburi ya halaiki na inaleta pamoja matawi ya sheria za kimataifa ambayo yanathibitisha ulinzi na ulinzi halali na juhudi za uchunguzi kwa njia zilizoundwa ili kunufaisha utumiaji wa familia wa haki zao za kibinadamu kwa ukweli na haki kwa ushirikiano

wenye nguvu wa kanuni, viwango na sheria mbalimbali za haki za kibinadamu zinazotumika kwa makaburi ya halaiki, utunzaji wa mabaki ya binadamu na masilahi ya familia zilizoathiriwa, manusura, jamii na mataifa. Inapotumika, Itifaki itasaidia kuhakikisha kuwa makaburi ya halaiki, na mabaki ya binadamu yaliyomo, yapokea utunzaji wenye heshima, usio na ubaguzi na wenye hadhi yanayostahili kutoka hatua ya ugunduzi wa mwanzo na uchunguzi hadi juhudi za utambuzi, na kuendelea kutekeleza haki kamili na maadhimisho ya muda mrefu. Kama jamii ya kimataifa, utunzaji wetu wa makaburi ya halaiki mara nyingi haukuwa unaofaa, wenye ubaguzi au, kwa urahisi kabisa, bila kujali. Hii inapaswa kukoma. Tunaweza na lazima tufanye vizuri zaidi na zaidi, kuheshimu na kulinda masilahi na wasiwasi mbalimbali wa familia, waathirika, jamii na kumuiya. Ni jukumu letu la pamoja kwa ubinadamu wetu wa kawaida.

Mamlaka ya Mwandishi Maalum kuhusiana na Mauaji ya Kiholela, Yasiyo ya Haki au Yasiyo na Msingi 2

Dak. Agnes Callamard Mwandishi Maalum wa UN kuhusu Mauaji ya Kiholela, Yasiyo ya Haki na Yasiyo na Msingi


Yaliyomo

Lengo na upeo wa Itifaki

Lengo na wupeo wa Itifaki......................................................... 3 Kanuni kuu za utendaji katika ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki....................................................................... 6 A. Ugunduzi na kuripoti salama................................................ 8 B. Ulinzi............................................................................................. 8 C. Uchunguzi.................................................................................... 9 D. Utambuzi...................................................................................... 12 E. Kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu.............................. 14 F. Haki................................................................................................ 15 G. Ukumbusho................................................................................. 16 Kiambatisho cha 1......................................................................... 17 Kiambatisho cha 2......................................................................... 18 Kiambatisho cha 3......................................................................... 19 Kiambatisho cha 4......................................................................... 20 Kiambatisho cha 5......................................................................... 21 Kiambatisho cha 6......................................................................... 22

Makaburi ya halaiki ni historia ya mara kwa mara inayotokana na migogoro na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Kwa walionusurika, hitaji la kujua hatima na mahali walipo wapendwa wao, na kupokea mabaki ya mauti kwa ajili ya mazishi na/au ukumbusho wa heshima, yanaweza kuwa makubwa sana. Kwa kuongezeka hitaji hili linatambuliwa kama haki ya kisheria ya kujua ukweli. Makaburi ya halaiki yana ushahidi ambao ni muhimu kwa utimilifu madhubuti wa ukweli, haki na uwajibikaji wa wahusika. Sheria na taratibu madhubuti za ulinzi, utunzaji na uchunguzi wa makaburi ya halaiki ni muhimu sana. Kwa sasa, hata hivyo, ingawa kuna mbinu kadhaa bora za utendaji zinazotumika miongoni mwa wahusika mbalimbali katika uwanja, hakuna viwango vya jumla vilivyopo, vya pamoja au vya kawaida. Kupitia mchakato shirikishi na wa mashauriano, Itifaki hii inajaza pengo hilo. Hairudufu wala kuchukua nafasi ya hati zilizopo kuhusiana na kanuni na mazoea mazuri1. Badala yake inatoa mbinu ya kuunganisha ya ndani na nje ya utaalamu kwa ulinzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi. Inafuata mpangilio wa michakato hii kwa ukamilifu pamoja na washikadau, taaluma na mifumo mingi inayoungana kwa madhumuni ya pande mbili, na yanayoimarisha pande zote za kukuza ukweli na haki, kwa kutoa: (1) Itifaki ya Kimataifa kuhusu Ulinzi na Uchunguzi wa Makaburi ya Halaiki, yenye msingi wa sheria zinazohusika, na kuchanganya na kuunganisha matawi ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, sheria ya kimataifa ya kibinadamu na - pale inapofaa - sheria ya kimataifa ya uhalifu; na Angalia orodha ya hati husika katika Kiambatisho cha 1.

1

@GraveProtection

massgraveprotection@bournemouth.ac.uk

www.bournemouth.ac.uk/mass-grave-protection

3


(2) Maoni ya Kielimu kuhusu Itifaki, yanayozingatia msingi na majadiliano ambayo yalisababisha sheria mbalimbali zilizomo. Maoni ya Kielimu, yaliyochapishwa kando, yanaangazia na kupanua mitazamo tofauti na mahitaji ambayo yanatokea katika mchakato wa ulinzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi ili kuhakikisha kuwa, katika utekelezaji, yanatarajiwa na, inapowezekana, kupunguzwa. Watumiaji: Itifaki imekusudiwa kutumiwa na wataalamu, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu: maafisa wa serikali na taifa, watekelezaji sheria, wawakilishi wa sheria, wataalamu wa uchunguzi, wataalamu wa afya, wataalamu wa usalama na wahusika wataalamu wa mashirika ya kijamii.2 Upeo na matumizi ya Itifaki: kulingana na kisa maalum Msamaha wa muktadha wa Itifaki hii umewekewa kikomo kwa makaburi ya halaiki ambayo huibuka katika muktadha wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na migogoro, ya ndani na ya kimataifa. Hii haiondoi, hata hivyo, Itifaki hiyo kuwa ya umuhimu kwa makaburi ya halaiki yanayotokana na hali tofauti.3 Waathiriwa katika makaburi ya halaiki wanaweza kuwa wanaume, wanawake na/au watoto. Wanaweza kuwa raia na/au wapiganaji wenye silaha kutoka pande zote za mgogoro. Itifaki imekusudiwa kutumika bila ubaguzi na bila kujali maoni ya kisiasa au maoni mengine, ushirikiano na wachache katika kitaifa, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa jinsia, dini au imani, umri, mbari, rangi, lugha, kabila, tabaka, asili ya kitaifa au kijamii, ulemavu wa mwili au akili, hali ya afya, mali, kuzaliwa, hali ya ndoa, au sababu nyingine yoyote inayotambuliwa na vyombo vya kisheria vya kimataifa. Hakuna jambo kama uchunguzi au ufuakuaji wa kaburi la halaiki wa ‘kawaida’. Uchunguzi kaburi la halaiki unazingatia muktadha mahususi. Hii inaweza kuwa kwa sababu kama vile mamlaka ya kijiografia na ya muda na pia mazingira ya kisiasa. Kwa sababu hiyo, Itifaki hii haikusudiwi kuwa kama maelekezo kulingana na mazoea bora katika visa vyote vya makaburi ya halaiki. Badala yake, Itifaki inatoa mazingatio maalum ambayo yamekusudiwa kusaidia na kuwaelekeza wahusika wanaposhughulika na mchakato wa uchunguzi katika uwezo wao mbalimbali na katika hatua zote. Kufikia mwisho huu, inapaswa kutambuliwa kuwa huenda mazingatio yaliyomo katika Itifaki yasiweze kutumika kwa kikamilifu kwa kila uchunguzi. Ijapokuwa Itifaki imeundwa kusaidia kwa msingi jumla, ubainishaji wa matumizi ya mambo mahusuzi ya Itifaki unapaswa kufanywa na mtaalam kwa msingi wa kila kisa.

Kando na hayo, kwa kiwango cha chini, na kulingana na njia, viwango vya uchunguzi na ulinzi vinavyotumika kwa hali yoyote vinapaswa kutosha kutimiza malengo ya ukweli na haki, yaani, vinapaswa kuhimili uchunguzi wenye mamlaka. Mbinu Yaliyomo katika Itifaki yameundwa kutokana na uzoefu na maoni ya wataalam walioalikwa, ikiwa ni pamoja na wataalam wa uchunguzi, wachunguzi, majaji, waendesha mashtaka, wahudumu wa usalama/polisi, wawakilishi wa asasi za kiraia na wasomi, wakiangazia kuhusu uzoefu wa ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki, utaalamu katika haki za binadamu, sheria za kibinadamu na/au uhalifu, pamoja na utofauti wa kijiografia.4 Ufafanuzi Kwa madhumuni ya Itifaki, tunatoa ufafanuzi ufuatao unaotumika: • Neno kaburi la halaiki, ambalo halijafafanuliwa katika sheria ya kimataifa, linatumika hapa kumaanisha ‘eneo au mahali palipobainishwa penye watu wengi (zaidi ya mmoja) wa waliozikwa, waliozama au sehemu iliyo na mabaki ya wanadamu yaliyotawanyika (ikiwa ni pamoja na mabaki ya mifupa, yaliyochanganyika na kugawanyika), ambapo hali kuhusiana na vifo na/au njia ya utupaji mwili inahitaji uchunguzi juu ya uhalali wake’. • Watu waliopotea inamaanisha ‘watu waliopotea kutokana na migogoro, ukiukwaji wa haki za binadamu na/au vurugu zilizopangwa.’5 • Kwa mwathiriwa Itifaki inamaanisha ‘watu ambao, mmoja au kwa pamoja, wameumia, ikiwa ni pamoja na kuumia kimwili au kiakili, mateso ya kihisia, kupoteza uchumi au kuathiriwa pakubwa kwa haki zao za kimsingi, kupitia vitendo au ukiukaji ambavyo vinakiuka sheria za uhalifu zinazotumika katika Taifa au kutokana na vitendo ambavyo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za binadamu za kimataifa au ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa sheria ya kibinadamu’.6 Sambamba na sheria za kimataifa, ufafanuzi wa mwathiriwa uliotumiwa katika Itifaki haujumuishi tu watu walio katika kaburi la halaiki (‘msingi’ Au waathiriwa wa ‘moja kwa moja’), lakini pia familia zao na, pale inapofaa, jamii (‘ wa pili’ au ‘wahanga’ wasio wa moja kwa moja). Kwa ajili ya uwazi, Itifaki hii pia inarejelea ‘familia’, ‘wanafamilia’ na ‘jamii zilizoathiriwa’ ambapo sheria fulani zinawahusu.7

Hii inaweza kujumuisha mipango ya uchunguzi wa kiraia ambapo inakuwa chini ya udhamini wa shirika lililoidhinishwa la utaalamu wa asasi ya kiraia. Mipango ya kisiasa pia inaweza ‘kuhalalisha’ manusura ambao wanaweza kushiriki katika mchakato wa uchunguzi na ufukuaji wa maiti na ambao huenda si wataalamu lakini wanatekeleza ufukuaji. Kwa majadiliano zaidi, angalia Maoni ya Kielimu yaliyoambatishwa. 3 Mfano, majanga, ikiwa ni pamoja na majanga yanayotokana na wanadamu na vifo vinavyotokana na utekelezaji wa mipaka au usafirishaji haramu. 4 Maelezo kuhusu mbinu ya sampuli ya ushiriki wa wataalam inaweza kupatikana katika Maoni ya Kielimu. 5 Imechukuliwa kutoka kwa Muungano wa Mabunge na ICRC (2009), Watu Waliopotea -Mwongozo wa Wabunge katika ukurasa wa 9 na kulingana na jukumu la Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea. Kama ilivyo kwa makaburi ya halaiki, hakuna fasili moja ya watu waliopotea. Ufafanuzi uliopendekezwa hapa ni finyu katika dhana kuliko ile inayopatikana katika Azimio la Baraza la Usalama la UN la 2019 kuhusu Watu Waliopotea kutokana na Vita vya Silaha, ambayo inaunga mkono ufafanuzi wa UNHCR wa 2010 wa watu ‘wasiowajibikiwa kutokana na vita vya silaha vya kimataifa au visivyo vya kimataifa’ tu (aya ya 9). Wakati huo huo ufafanuzi hapa haujumuishi kwa uwazi wahamiaji waliopotea, mada ambayo haiwezi kuangaziwa kikamilifu na Itifaki. 6 Huu ni ufafanuzi uliojumuishwa kutoka Azimio la Umoja wa Mataifa la Kanuni za Msingi za Haki kwa Waathiriwa wa Uhalifu na Matumizi Mabaya ya Mamlaka, kwenye Kiambatisho cha A, 1, na Kanuni za Msingi za UN na Miongozo juu ya Haki ya Suluhisho na Malipo kwa Waathiriwa wa Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, Kiambatisho cha V, 8, na inaunga mkono kifungu cha 24(1) cha Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote kutokana na Upoteaji Unaotokana na Mamlaka. 7 Ambapo kuna rejeleo dhahiri kwa ‘familia’, ‘wanafamilia’ au ‘jamii zilizoathiriwa’, hii haikusudiwi kwa njia yoyote kuashiria kwamba wao pia sio waathiriwa. Aidha, inatambuliwa kuwa familia binafsi na wanajamii wanaweza kuwa waatjiriwa wa moja kwa moja wa madhara mengine yaliyosababishwa katika muktadha mpana wa ukiukaji unaochunguzwa, ambapo makaburi ya halaiki ni sehemu yake. 2

4


• Neno familia, ambalo halina ufafanuzi katika sheria ya kimataifa, limetumika hapa kama dhana inayohusiana na mazoea ya jamii katika muktadha mahususi.8 Kwa madhumuni ya Itifaki hii, ushirika wa familia ni muhimu kwa kubaini, kwa mfano, jamaa wa karibu9, mpokeaji anayefaa ya mabaki ya mauti na utoaji wa hati za hali ya kisheria kwa heshima ya mtu aliyepotea. Ushirika wa familia unapaswa kubainishwa kulingana na sheria za eneo, mila na/au mazoea. • Uchunguzi wa kisheria (sawa na maana yake halisi ‘katika korti wazi’ au ‘umma’) inamaanisha eneo la kisayansi, kisheria na kijamii kwa kuleta maswala katika na mbele ya korti za kisheria na/au njia zingine za kimahakama (kama vile afisa mchunguzi wa vifo). Muundo wa Itifaki Hati inajumuisha michakato mbalimbali ya mpangilio inayotumika kwa ulinzi na uchunguzi wa kaburi la halaiki wakati huo huo ikifuata mbinu ya kawaida, kwa hivyo yaliyomo kwenye Itifaki yana msingi wazi katika sheria na kanuni za kisheria za kimataifa. Kila sehemu kwa hivyo itaanza na kisanduku cha bluu kikielezea sheria za msingi zaa kanuni kutoka kwa sheria ya kimataifa10 (kanuni za kimataifa) na hivyo kutoa mantiki ya kisheria kwa yaliyomo yaliyopendekezwa ya Itifaki. Msingi wa kisheria Sehemu ya kuanza kwa Itifaki kwa ujumla ni wajibu wa Mataifa kutafuta na kuchunguza. Kanuni za kimataifa Wajibu wa kutafuta na kuchunguza Chini ya sheria za haki za binadamu, Mataifa yana wajibu wa kutafuta na kuchunguza wakati haki ya mtu binafsi, na ulinzi wake, umekiukwa. Haki ya kuishi na marufuku ya mateso au matendo mengine ya kikatili, yasiyo ya kibinadamu au ya kudhalilisha ni pamoja na utaratibu unaohitaji uchunguzi madhubuti (ICCPR11, Kifungu cha 6 na 7). Chini ya sheria za kieneo za haki za binadamu, uchunguzi lazima uwe wa haraka, huru, kamili, bila upendeleo na wenye uwazi. Matokeo yake lazima yawe na msingi ‘kulingana na uchambuzi wa kina, madhubuti na usio na upendeleo wa mambo yote muhimu.’12

Kifungu cha 24(3) cha Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Watu Wote kutokana na Upoteaji Unaotokana na Mamlaka (CED13) kinahitaji Washirika wa Taifa ‘kuchukua hatua zote zinazofaa ili kutafuta, kupata na kuwaachilia watu waliopotea na, katika tukio la kifo, kupata, kuheshimu na kurudisha mabaki yao’. Ni wajibu unaoendelea hadi hatima na/ au mahali walipo wale waliopotea pamegunduliwa (Kanuni za Kuongoza za CED14, Kanuni ya 7). Kwa ujumla, jukumu la kufanya uchunguzi madhubuti ni wajibu wa njia na sio wa matokeo.15 Sheria ya kimataifa ya kibinadamu inahitaji kutafutwa kwa wafu (kwa mfano, GC I, Kifungu cha 15; GC II, Ibara ya 18 na 21; GC IV, Kifungu cha 16; Itifaki ya Ziada ya I, Kifungu cha 17(2)) na waliopotea (Itifaki ya Ziada ya I, Kifungu cha 33 (2))16. Sheria ya kitamaduni ya kibinadamu ya kimataifa inapendekeza kila mshirika kwenye mgogoro, uwe wa kimataifa au wa ndani, ana wajibu wa ‘kuchukua hatua zote zinazowezekana kuwajibika kwa watu walioripotiwa kupotea kutokana na vita vya silaha’ (Kanuni za CIHL17 2006, Kanuni ya 117). Wakati tukikubali kwamba makaburi ya halaiki yanaweza kuwa katika mazingira yenye vifaa finyu au yasiyo na upatikanaji wa mbinu, mahakama iliyolemewa, ukosefu wa usalama na idadi kubwa ya mahitaji tofauti, ya wakati mmoja, kuna mahitaji wazi ya sheria ya ndani na uanzishwaji wa taasisi mahususi. Sheria na taasisi kama hizo zinachukuliwa kama sharti la jibu madhubuti kwa visa vyote vya watu waliopotea. Kanuni za kimataifa: Sheria ya Watu Waliopotea na Mamlaka mahususi ya Watu Waliopotea CED inahitaji mamlaka husika kuwa na rekodi na sajili rasmi za watu wote walionyimwa uhuru wao (Kifungu cha 17 (3)). Usimamizi wa sajili na hifadhidata unapaswa kuheshimu faragha ya wahasiriwa na usiri wa maelezo (Kanuni ya Kuongoza ya CED, 11(8)).

Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea hutumia neno ‘jamaa wa watu waliopotea’ kwa kurejelea, na kwa mujibu wa, masharti ya sheria ya ndani inayotumika (Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) (2009), Kanuni za Kuongoza/Sheria ya Mfano kuhusu Waliopotea, Kifungu cha 2(2)) (kwa kifupi Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea). 9 Ikiwa ni pamoja na uhusiano wa kijeni na jamaa wa karibu (Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 273 na 274. 10 Orodha ya masharti ya kawaida inaweza kuwa ya kuonyesha tu. 11 Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (uliopitishwa 19 Disemba 1966, ulianza kutumika tarehe 23 Machi 1976) 999 UNTS 171 (kwa kifupi ICCPR). Angalia pia Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (HRC), Maoni ya jumla nambari 36, Kifungu cha 6 (Haki ya Kuishi) CCPR/C/GC/35 (3 Septemba 2019) aya ya 58. 12 Kukhalashvili and others v Georgia, Hukumu, Maombi ya ECtHR nambari 8938/07 na 41891/07 (2 Mei 2020) aya 130. 13 Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote Kutoka kwa Upoteai Unaotokana na Mamlaka (uliopitishwa 12 Januari 2007 ulianza kutumika 23 Disemba 2010) Hati ya UN ya A/RES/61/177 (20 Disemba 2006) (kwa kifupi CED). 14 Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Upoteaji Unaotokana na Mamlaka, Kanuni za Kuongoza katika kutafuta watu waliopotea (8 Mei 2019) Hati ya UN ya CED/C/7, Kanuni ya 7 (baadaye hapa ni Kanuni za Kuongoza za CED). 15 Da Silva v United Kingdom, Hukumu ya Baraza Kuu, Maombi ya ECtHR Nambari 5878/08 (30 Machi 2016) vifungu vya 231-238, inatoa muhtasari kamili wa Baraza Kuu wa mahitaji ya uchunguzi madhubuti. 16 Mkutano wa Geneva (I) kwa Uboreshaji wa Hali ya Waliojeruhiwa na Wagonjwa katika Vikosi vya Wanajeshi Vitani (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 31 (kwa kifupi GC I); Mkutano wa Geneva (II) wa Uboreshaji wa Hali ya Wanajeshi Waliojeruhiwa, Wagonjwa na Wahasiriwa wa Jeshi wa Meli Zilizovunjika Baharini (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 85 (kwa kifupi GC II); Mkutano wa Geneva (IV) unaohusiana na Ulinzi wa Wananchi katika Wakati wa Vita (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 288 (kwa kifupi GC IV); na Itifaki ya Ziada ya Mikataba ya Geneva ya tarehe 12 Agosti 1949, na Kuhusiana na Ulinzi wa Wahasiriwa wa Migogoro Vita vya Silaha ya Kimataifa (Itifaki I) (iliyopitishwa tarehe 8 Juni 1977, ilianza kutumika tarehe 7 Disemba 1979) 1125 UNTS 17512 (kwa kifupi Itifaki ya Ziada). 17 Henckaerts J-M. na Doswald-Beck L., (2006) Sheria ya Kimila ya Kibinadamu ya Kimataifa,Toleo la 1: Kanuni (kwa kifupi Kanuni za CIHL). 8

5


Mamlaka iliyoteuliwa ya Watu Waliopotea kwa uratibu wa juhudi za watu waliopotea (Sheria ya Bosnia kuhusu Watu Waliopotea18 Kifungu cha 7, angalia pia Kanuni ya Kuongoza ya CED 12(1) na 12(3)) na utaalam unaofaa unaohitajika, unapendekezwa, kujumuisha jukumu la kulinda kaburi la halaiki, uchunguzi na urejeshaji wa mabaki ya binadamu. Inapaswa pia kutoa njia salama za kupokea maombi ya ufuatiliaji (Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea19, Kifungu cha 12 na 12(3)) na kuunda sajili ya watu waliopotea na maelezo yanayohusiana. Azimio la Baraza la Usalama la UN la 2019 linasisitiza hitaji la ‘kutunga sheria’ (UNSC 247420 katika ukurasa wa 2) katika kiwango cha ndani ili kukabiliana na suala la watu waliopotea. Sheria inapaswa kuwa isiyo ya ubaguzi, inayihakikisha ulinzi, uchunguzi na utambulisho wa watu wote kwa kiwango kamili iwezekanavyo. Wakati mamlaka ya kitaifa huenda isiwe kila wakati na miundo iliyopo ya kushughulikia hali za kipekee za makaburi ya halaiki kabla ya mgogoro, udhalimu wa haki za binadamu au majanga, bado kuna uwezekano wa kuwa na baadhi ya mifumo wa kisheria inayotumika ambapo michakato inatawaliwa na sheria, kanuni na mazoea ya nchi iliyoathiriwa.21 Isipokuwa kama jukumu la kisheria la kimataifa linachukua nafasi ya kwanza, heshima na uzingatiaji wa kanuni hizi za kisheria zitatumika kwa wahusika wote. Zitasimamia maswala ya nani ana haki ya kutafuta watu waliopotea na kudai uchunguzi wa makaburi ya halaiki, na itaamuru kurejeshwa kwa michakato ya mabaki ya binadamu. Ujumbe wa tahadhari kuhusu ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki Licha ya uwepo wa haki za kisheria, uchunguzi wa kaburi la halaiki ni jukumu la njia na sio matokeo (yaani, juhudi bora na huru kutokana na rasilimali zilizopo). Uchunguzi wa kaburi la halaiki kawaida ni mchakato mgumu sana, mrefu na wa gharama kubwa, unaohitaji mipango muhimu, uratibu, rasilimali, idhini rasmi na utashi wa kisiasa. Uchunguzi wenyewe unaweza kuathiri wadau wengi, ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, waathiriwa binafsi na familia; mashahidi; vikundi vya wahasiriwa; jamii zilizoathirika; mashirika ya utaalamu; NGO; mamlaka za mitaa, eneo na kitaifa mamlaka na mashirika ya kitaifa; na huluki za kimataifa kama vile tume za uchunguzi za UN na mashirika ya kimataifa. Kwa hivyo, kutakuwa na masilahi na mahitaji anuwai ya kibinafsi, ya pamoja na ya kijamii, ambayo huenda yasioane au kupatanishwa kwa urahisi. Aidha, katika hali ya kiwango kikubwa, huenda isiwezekane kupata, kutambua na kurejesha waathiriwa wote kutoka kwenye kaburi la halaiki, na hii inaweza kuwa na athari kwa familia za jamii za watu waliopotea na kuathiriwa.

Inaweza pia kuathiri mitazamo ya haki na shughuli za kutafuta haki katika ndani na nje ya nchi, ambapo kufukuliwa kwa maiti ni sehemu ya mchakato wa kimahakama.22

Kanuni kuu za utendaji katika ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki Kwa kuongezea mambo yaliyoonyeshwa katika Itifaki hii ambayo inatumika katika hatua mbalimbali za mchakato wa ulinzi na uchunguzi, kuna kanuni kadhaa kuu za kiutendaji ambazo zinapaswa kuelekeza na kuongoza mchakato(michakato) huu kwa jumla, ikitumika katika hatua zote, kwa wahusika wote, katika viwango vya kitaifa na kimataifa. Ingawa zimeorodheshwa kando hapo chini, zinahusiana katika mazoea. (1) Usidhuru Mbinu ya ‘usidhuru’ inaungwa na kanuni zingine zote za utendaji, na inahitaji uelewa wa njia zinawezekana ambazo uwepo na mwenendo wa uchunguzi wa kaburi la halaiki unaweza kuathiri muktadha na mazingira pana, pamoja na kuthamini njia ambayo athari hasi zinaweza kuepukwa na/au kupunguza kila inapowezekana. Kama uingiliaji katika haki za binadamu, migogoro na mazingira ya baada ya migogoro, shughuli kama hizo kwa asili zinaunda sehemu ya mienendo pana ya muktadha wa utendaji wake. Jamii zinaweza kuwa zinapitia mabadiliko ya haraka, ambayo yanaweza kujumuisha kiwango kinachoendelea katika miundo ya kijamii na nguvu na kuanzisha upya kwa kanuni za kijamii. Mbinu ya “Usidhuru” katika mazingira haya itatafuta kabisa kuzuia kudhoofisha miundo na uhusiano uliopo ambao ni muhimu kwa uundaji wa ya amani na utangamano wa jamii. Inapaswa pia kuzuia kuunda hali ya kutokuwa na usawa au mitazamo yenye upendeleo au upendeleo, ikiwa ni pamoja na kuhusiana na hali na rasilimali, au kusisitiza hali zilizopo za kutokuwa na usawa, ikiwa ni pamoja na kuhusiana na jinsia. Itajumuisha heshima ya wazi kwa na, na inapowezekana, kuzingatia unyeti na mila za kitamaduni, na imani zinazojulikana za kidini za wahasiriwa na/au familia zao inapaswa kuzingatiwa kwa kadiri inavyowezekana na kwa kiwango ambacho haziathiri vibaya mafanikio ya uchunguzi madhubuti. (2) Usalama wa mwili na kihisia Usalama wa mwili na kihisia wa timu ya uchunguzi, familia za waliopotea, mashahidi na mshirika mwingine yeyote anayehusika na uchunguzi ni muhimu. Usalama, utu, faragha na ustawi wa waathiriwa na familia zao unapaswa kuwa jambo muhimu kwa wahusika wote bila ubaguzi. Hii inaweza kuhitaji mipango ya kusaidia usalama wa mwili na kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na kutoa rufaa zinazofaa na kutumia kwa mbinu zinazozingatiwa wakati wa kufanya mahojiano na watu walio na uwezekano wa kuwa na kiwewe. Aidha, uangalifu unapaswa kuzingatiwa ili kupunguza na kukabiliana na visa vya viwewe vibaya na athari zingine mbaya za kihisia kwa washirika wa timu.23

Bosnia na Herzegovina: Sheria kuhusu Watu Waliopotea (21 Oktoba 2004), Gazeti Rasmi la Serikali ya Bosnia na Herzegovina 50/04. Mfano wa Sheria wa ICRC kuhusu Waliopotea. 20 UNSC, Azimio 2474, la 11 Juni 2019, Hati ya UN ya S/RES.2474. 21 Angalia, kwa mfano, Mwongozo wa Utambulisho cha Waathiriwa wa Majanga wa Interpol (2018), Sehemu ya B, Kiambatisho cha 1, katika kifungu cha 4.1. 22 Afisa wa ushirikiano wa kifamilia na jamii, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa matarajio unashughulikiwa kwa undani zaidi hapo chini, katika kanuni kuu na katika Sehemu ya C ya Itifaki hii. 23 Angalia, kwa mfano, OHCHR, Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu, Sura ya 12, ambayo inajumuisha mwongozo wa kina kuhusu jinsi ya kufanya mahojiano na watu walio na kiwewe, na pia huduma za utunzaji kibinafsi. 18 19

6


Mikakati na shughuli mahususi za ulinzi zinapaswa kuendelezwa. Umma unapaswa kufahamishwa kuhusu uwepo wa hatua za ulinzi ili kutoa uhakikisho na kuhamasisha ushiriki wao katika uchunguzi. Ambapo hali ya usalama iliyopo inaruhusu, yaliyomo mahususi ya hatua za ulinzi kuhusiana kwa familia za waathiriwa na mashahidi wanaotarajiwa pia yanaweza kuwekwa katika miliki ya umma. Wale wanaohusika moja kwa moja na uchunguzi wowote wanapaswa kufahamishwa kuhusu yaliyomo ya hatua zinazofaa za ulinzi, ikiwa ni pamoja na vizuizi vyovyote kuhusiana na mfumo wa ulinzi unaotolewa ili hatua yoyote kuhusika katika uchunguzi itegemee uamuzi sahihi. Kuheshimu utu wa waathiriwa ni pamoja na utunzaji wa heshima na uangalifu wa mabaki ya binadamu. Suala la usalama linapaswa kuzingatiwa. (3) Uhuru na kutopendelea Njia isiyo ya ubaguzi na isiyo na upendeleo inapaswa kutumika kwa wote.24 Ili uchunguzi utambuliwe kuwa halali machoni mwa jamii iliyoathiriwa, na kwa hivyo kuongeza ushiriki wa jamii, usaidizi wa sheria na uwajibikaji wa umma, timu yoyote ya uchunguzi haifai tu kufanya kazi kwa uhuru na bila upendeleo, lazima waonekane wakifanya hivyo. Kwa kadiri inavyowezekana, timu za uchunguzi zinapaswa kuepuka, kuzuia au kupunguza hali ambazo zinaweza kusababisha shughuli zao kuonekana kuwa na upendeleo na kuwa na udhibiti wa mitazamo ya kisiasa, kidini au kikabila. Inapaswa ikumbukwe, hata hivyo, kwamba makaburi ya halaiki kawaida hufanyika katika mazingira ya kisiasa na/au ya kitamaduni yenye hisia nyingi, ambayo inaweza kuwa ikiendelea wakati wa uchunguzi. Kutokana na hili, timu za uchunguzi zinapaswa kujua kuwa kufukuliwa kwa kaburi fulani kunaweza, kwenyewe, kusababisha mitazamo ya upendeleo katika baadhi ya sekta za jamii. (4) Usiri Uhakikisho na heshima ya usiri kuhusiana na maelezo ya kibinafsi na data nyingine ya utambulisho zinaweza kuwa muhimu katika kujenga uaminifu na, kuhakikisha usalama wa, familia za waathiriwa wanaoshukiwa, na zinaweza kuwa muhimu katika kuhakikisha kuripotiwa kwa maeneo ya makaburi ya halaiki, utambulisho wa jamaa waliopotea na utoaji wa data ya watu waliopotea na sampuli za marejeleo ya DNA. Taratibu za usiri zinapaswa kuwekwa, kueleweka na kutumiwa na washiriki wote wa timu ya uchunguzi. Masharti ya taratibu za usiri yanapaswa kuambatana na masharti ya kitaifa, na kufahamishwa kwa jamii zilizoathiriwa na kutolewa kwa umma. Familia za waliopotea na wanajamii wengine wanapaswa pia kufahamishwa kuhusu mipaka ya taratibu za usiri. Ambapo utambulisho na/au michakato ya uchunguzi inahusu hitaji au wajibu kwa kushiriki data, mchakato, asili na madhumuni ya kushiriki inapaswa kuwekwa wazi katika hatua ya mwanzo iwezekanavyo. Ushiriki wowote wa data unapaswa kuwa tu kwa wale watu na mashirika muhimu ili kuhakikisha kutimizwa kwa malengo ya mchakato wa kufukua mwili, na kwa kiwango kinachokubaliwa na watu husika.

(5) Uwazi Hatua zote za mchakato wa uchunguzi, ufukuaji wa maiti, utambulisho na urejeshwaji wa mabaki ya binadamu unapaswa kuwa wazi kwa kadri inavyowezekana kwa pande zote zinazohusika katika juhudi za ulinzi na uchunguzi, familia za waliopotea na umma. Uwazi utasaidia kuunga mkono mchakato wa uchunguzi wa umma. Uanzishwaji wa taratibu na itifaki rasmi zilizo wazi, zenye uwazi na zinazopatikana ili kuongoza mchakato zitakuwa muhimu. Pale ambapo wataalamu ni washiriki wa vyombo vya kisheria/mashirika ya kisheria, michakato ambayo mashirika hayo yanathibitisha uwezo wa washirika pia inapaswa kupatikana na kuwa na uwazi ili kuimarisha mitazamo ya umma na familia kuhusu uaminifu wa wataalamu. Ambapo inatumika, idhini maalum ya maabara ya kisayansi inayotumiwa kwa uchunguzi wa sampuli za binadamu au vifaa inapaswa kupatikana, pamoja na taratibu zozote zilizopo za kisayansi, kiufundi na kiutawala zilizopitishwa na maabara. Vizuizi vyovyote kuhusu uwazi vinapaswa kuwa muhimu sana, zinazolingana na haki za waathiriwa na familia zao kuhusiana na utu na usiri, na kutekeleza kusudi halali, ikiwa ni pamoja na usalama wa wahusika wote na wahusika wanaowezekana wanaohusika. (6) Mawasiliano Kuanzishwa mapema na kudumishwa kwa mikakati na njia za mawasiliano (pamoja na kupitia mitandao ya jamii) na jamii iliyoathiriwa, vyombo vya habari na umma kwa mapana zaidi ni muhimu kwa uwepo wa uaminifu, nia njema na uhalali wa shughuli hiyo, na itawezesha utoaji mwingine wa mambo muhimu, ikiwa ni pamoja na kuripoti - katika maeneo ya makaburi na waliopotea - vile vile kama ushiriki na michakato ya utambulisho na uchunguzi. Mawasiliano wazi na inayoendelea pia hutoa jukwaa la uwazi. Mikakati ya mawasiliano inapaswa kuzingatia na kujumuisha mtiririko wa maelezo wa njia mbili, na ujumuishe taarifa za mara kwa mara. (7) Matarajio halisi Familia za waliopotea zinaweza kuwa na matumaini makubwa kwamba wapendwa wao watatambuliwa na kurejeshwa kwao kwa ukumbusho wa heshima. Katika utekelezaji, hata hivyo, utambulisho na urejeshaji wa mabaki ya binadamu huenda usiwezekane kila wakati, na matarajio yanapaswa kudhibitiwa iwezekanavyo ili kuhakikisha ushiriki na usaidizi unaoendelea kwa mchakato wa kufukua maiti. Ugumu unaweza kushuhudiwa haswa katika hali ambazo ukatili umefanywa kwa kiwango kikubwa, ambapo kuna umati wa makaburi mengi ya halaiki na watu waliopotea, ambapo makaburi hayajagunduliwa na/au ambapo uwezo na rasilimali chache zina uwezekano wa kudhibiti juhudi za kufukua na/au utambulisho. Washirika wote wanaohusika katika ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki wanapaswa kuepuka kutoa ahadi kwa familia ambazo wanaweza kushindwa kutimiza.

Kwa kweli, hii inaweza kuhusisha kupitishwa kwa mbinu tofauti za uchunguzi katika visa vya, kwa mfano, wanawake, wazee, watu na/au watoto walio na kiwewe, ambapo ukosekanaji wa usawa wa kweli au matatizo yapo katika utekelezaji.

24

7


A. Ugunduzi na kuripoti salama Kanuni za kimataifa Chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, CED inahitaji utekelezaji wa ndani wa haki adilifu ya kuripoti, ili kuhakikisha mtu anayedai upoteaji unaotokana na mamlaka umetokea anaweza kuripoti ukweli kwa mamlaka zinazostahiki wakati huohuo akipewa ulinzi unaofaa (Kifungu cha 12 cha CED(1)). Hata bila malalamiko rasmi, maadamu kuna sababu nzuri za kuamini upoteaji unaotokana na mamlaka umetokea, mamlaka zinahitajika kufanya uchunguzi (CED, Kifungu cha 12(2)). Chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, washirika kwenye mgogoro lazima warekodi maelezo yote yanayotambulisha kabla ya mazishi ya mabaki ya binadamu na kuweka alama eneo la kaburi (Kanuni za CIHL, Kanuni ya 116; GC IV, Kifungu cha 130). Kuanzishwa kwa uchunguzi wa kaburi la halaiki kunaweza kutegemea mamlaka kwanza kufahamishwa kuhusu uwepo wa kaburi la halaiki linaloshukiwa. Mifumo ya ndani inaweza hata kuainisha jukumu la kuripoti.25 Hata hivyo, ripoti kama hizo zinaweza kukosa kupatikana wakati wote ambapo ‘mtoa habari’ (ambaye anaweza kuwa au asiwe jamaa wa mtu aliyepotea) angependa kubaiki bila kutambuliwa na, au kujulikana na mamlaka. Kuripoti salama: Utoaji wa michakato salama ya kuarifu mamlaka inahitajika.26 Watu au mashirika yanaweza kuwa ya kwanza kugundua au kusikia ripoti kuhusu kaburi la halaiki linaloshukiwa. Ripoti inaweza kujumuisha au inapaswa kusababisha kurekodi eneo la kaburi la halaiki linaloshukiwa. Hii inaweza kupatikana kupitia huduma za kijiografia na zana za kurekodi uratibu na mahali ili kubainisha maeneo, kama vile: • Mfumo wa Kuweka Nafasi Ardhini (GPS) au Mfumo wa Marejeleo ya Mraba Fito wa Kijeshi (MGRS); • Ramani kwenye simu ya mkononi; • Data ya meta kutoka picha zilizopigwa kwenye simu mahiri. Kumbukumbu ya awali ya eneo inaweza kufanywa kupitia: • Picha; • Kurekodi video; • Maelezo yaliyoandikwa au sauti iliyorekodiwa kuhusu eneo; • Mchoro au utambulisho kwenye ramani. Hii inaweza kufanywa na wahudumu wa kwanza, maripota au wenyeji ambao wameona eneo linalowezekana.27 Hii inapaswa kufuatiwa na mashirika/maafisa wa uchunguzi kufanya tathmini ya mwanzo ya eneo.

Vifaa kama vile ndege za roboti, satelaiti na teknolojia zingine zisizo za uingiliaji, ambapo zinapatikana, zinaweza kusaidia zaidi katika kuweka kumbukumbu.

B. Ulinzi Kanuni za kimataifa Ili kufanya uchunguzi madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ukweli wa ushahidi uliopatikana kutoka eneo, ni muhimu kwamba kaburi la halaiki lisibadilishwe au kuharibiwa na watu wengine (ikiwa ni pamoja na wahudumu wa kwanza). Kifungu cha 12 cha CED(3) (a) kinaamuru kwamba mamlaka zina ‘nguvu na rasilimali muhimu za kufanya uchunguzi kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na ufikiaji wa kumbukumbu na maelezo mengine muhimu kwa uchunguzi wao’ (msisitizo umeongezwa). Sheria ya haki za binadamu inasisitiza bidii inayofaa na inapendekeza kwamba ‘mamlaka lazima zichukue hatua adilifu zinazopatikana kwao ili kupata ushahidi’.28 Chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, Kifungu cha 34(2) (b) ya Itifaki I ya Ziada inahitaji kulindwa kwa maeneo ya makaburi. Kuna haja pia ya ‘kuchukua hatua zote zinazowezekana kuzuia waliokufa kuharibiwa tena’, na uharibifu au uathiri wa maiti ni marufuku kabisa (Kanuni za CIHL, Kanuni ya 113; ICC St. Kifungu cha29 8(2)(b)(xxi) na 8(2)(c) (ii) kama uhalifu wa kivita); na utupaji wenye heshima wa maiti ikiwa ni pamoja na heshima na utunzaji wa makaburi (Kanuni ya 115) unahitajika. Kuiba kutoka kwa wafu, hata bila kosa lililoongezwa la kuua, ni uhalifu.30 Ulinzi wa eneo ni muhimu sana ili kudumisha uadilifu wa mabaki na ushahidi na mifumo ya uchunguzi lakini wakati huo huo unaweza kuvutia uangalifu wa kaburi la halaiki kama eneo la maslahi, na kuongeza hatari ya uharibifu wa ushahidi. Ufukuaji usio na utaalamu unaweza kusababisha uchanganyishaji, ukusanyaji usio na utaalamu wa ushahidi unaohitajika kwa madhumuni ya utambulisho na/au uchunguzi wa uhalifu, kushindwa kukusanya data kulingana na viwango vinavyofaa vya uthibitisho na kuongezeka kwa uharibifu wa maiti baada ya kufa. Urejeshaji usiofaa wa miili pia unaweza kuhusisha utunzaji usio na heshima (ikiwa ni pamoja na kutazama kwa umma) na kuzidisha kiwewe cha familia. Ulinzi unaweza kulinda dhidi ya picha zisizo na ruhusa za picha na za kusumbua zinazopigwa na kusambazwa.

Angalia, kwa mfano, Sheria ya Iraqi Nambari 13 ya 2015, Sheria ya Maswala na Ulinzi wa Makaburi ya Halaiki, kurekebisha Sheria Nambari 5 ya 2006, Ulinzi wa Makaburi ya Halaiki, Kifungu cha 9. Vivyo hivyo, Kanuni ya Uhalifu ya 2003 ya Bosnia na Herzegovina chini ya kifungu cha 231a inapiga marufuku hatua ya kutoripoti eneo la kaburi la halaiki kwa kifungo cha jela (Bosnia na Herzegovina: Kanuni ya Uhalifu (27 Juni 2003), Gazeti Rasmi la Serikali ya Bosnia na Herzegovina 37/03). 26 ICMP, kwa mfano, inatoa Kituo cha Uchunguzi cha Mtandaoni na kupitia Kionyesha Eneo chake mtu yeyote anaweza kuripoti kwa njia hii. 27 Global Rights Compliance (2016), Viwango vya Msingi vya Uchunguzi kwa Wahudumu wa Kwanza kwa Uhalifu wa Kimataifa. 28 Treskavica v Croatia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 32036/13 (12 Aprili 2016) aya ya 60, ikibainisha kuwa hii inajumuisha ushahidi wa uchunguzi wa kisheria. Maelezo kuhusu jinsi ya kukabiliana na eneo linalowezekana la uhalifu yamo katika Mwongozo wa 2011 kuhusu jinsi ya kusaidia uchunguzi wa uhalifu wa kimataifa katika kifungu cha 7.1 kuhusu Kulinda Eneo la Uhalifu, ukurasa wa 65. Itifaki za Minnesota zinasema kwamba ‘eneo la uhalifu linapaswa kulindwa mapema zaidi iwezekanavyo na wafanyakazi wasioidhinishwa hawapaswi kuhusiwa kuingia’ (ukurasa wa 14 katika aya ya 59). 29 Sheria ya Rome ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (iliyopitishwa tarehe 17 Julai 1998, ilianza kutumika tarehe 1 Julai 2002) 2187 UNTS 3 (kwa kifupi ICC St.). 30 Pohl et al. Mahakama ya Kijeshi ya Marekani katika Nuremberg (3 Novemba 1947). 25

8


Ulinzi pia unalinda mabaki ya binadamu dhidi ya uchafuzi, uchafuzi wa mazingira, wizi, watapeli na upelekaji/uhamishaji wa miili kwenda maeneo ya pili, ambapo mhalifu anataka kukwepa kugunduliwa. Kupitia bila ruhusa na kubadilisha kunaweza kuwa kosa la uhalifu katika mfumo wa ndani.31 Masharti ya kabla ya mfumo madhubuti wa ulinzi: • Uthibitishaji wa ripoti na ushahidi kupitia mbinu mbalimbali na vyanzo vingine. • Kuweka kwenye ramani na kuweka kumbukumbu za makaburi ya halaiki kulingana na kiwango chao na muktadha wa eneo yaliko. Hatua muhimu za ulinzi zinaweza kujumuisha: • Kulinda eneo na kudhibiti ufikiaji: ruhusa ya kisheria32 ya kufikia ardhi inapaswa kutafutwa na kupatikana. Hii inaweza pia kuhitaji ushirikiano wa jamii na idhini kwa utekelezaji. Ufikiaji unaweza kuathiriwa na uwepo wa maeneo muhimu ya kitamaduni, sababu za kijiografia na udhibiti. Hatari zinazopatikana kwenye eneo ni pamoja na vilipuzi ambavyo havijalipuka na uchafu. • Hatua za ulinzi zinaweza kujumuisha: uzio ili kulinda mzunguko wa nje; ufunikaji wa njia mlalo ili kulinda mabaki kwenye sehemu za juu na walinzi wa usalama na ufuatiliaji ndani ya eneo. Hatua kama hizo pia zinategemea urefu wa muda kati ya ugunduzi na uchunguzi, muktadha wa kieneo na hatari katika eneo (kwa mfano, kuwekwa katika hatari ya viasili na wanyama). Kulinda eneo kunaweza kuhitaji hatua za usalama kwa wale wanaotoa hatua za ulinzi, kwani maoni ya umma yanaweza kuwa dhidi yao. • Huenda ufikiaji halisi usiwezekane kila wakati kwa mfano ambapo wachunguzi hawawezi kuingia nchini. Ufuatiliaji ndani ya eneo kupitia picha za setilaiti inaweza kuwa njia pekee ya ulinzi inayopatikana. Ulinzi unapaswa kutolewa iwe eneo limebadilishwa au la.

C. Uchunguzi Kanuni za kimataifa Chini ya sheria za haki za binadamu ya jukumu la kufanya uchunguzi madhubuti inamaanisha kuwa uchunguzi unahitaji kuwa huru na wa kutosha (kwa mfano, Kifungu cha 12 cha CED), unaoweza kubaini ukweli na kutambua waliohusika.33 Hii ni pamoja na kupata ushahidi wa uchunguzi wa kisheria na uchunguzi wa maiti, kwa rekodi kamili na sahihi na uchambuzi huru wa majeraha na sababu ya kifo.34 Uchunguzi lazima uwe na mamlaka ya kutosha kupata maelezo na kuwawajibisha maafisa. Unapaswa kufanyika kwa haraka; kwa jumla, ni jukumu linaloendelea la kuchunguza35 lakini ni jukumu la njia na sio mwisho.36 Mahakama ya Marekani ya Haki za Binadamu inasisitiza hitaji la uchunguzi kuzingatia muktadha mpana na utata unaozunguka matukio37 ili kufikia ‘ukweli kamili zaidi wa kihistoria unaowezekana, ikiwa ni pamoja na ubainishaji wa mitindo ya hatua ya pamoja’38 kulingana na haki ya kujua ukweli (kwa mfano, Kifungu cha CED cha 24(2)). CED inabainisha zaidi katika kifungu cha 12(4) kwamba nchi wanachama zinapaswa ‘kuchukua hatua zinazohitajika za kuwekea vikwazo vitendo vinavyozuia kufanyika kwa uchunguzi. ‘Ambapo inafaa, hii inaweza kujumuisha ushirikiano wa kimataifa katika ya Mataifa na mashirika husika (Kanuni za Kuongoza za CED, Kanuni ya 3(4)). Uchunguzi unaofuatilia malengo ya kibinadamu tu huenda “kivyake usiweze kuwa wa kutosha kufikia kiwango cha uchunguzi madhubuti’ kama inavyotakiwa na Mkataba wa Ulaya Ibara ya 2.39 Kulingana na Kanuni za Orentlicher40; ‘[b]ila kujali kesi zozote za kisheria, waathiwa na familia zao wana haki isiyo na kikomo ya kujua ukweli kuhusu mazingira ambayo ukiukaji ulifanyika na, ikiwa kuna kifo au kutoweka, hatima ya waathiriwa’. Chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, familia zina haki ya kufahamishwa kuhusu hatima ya wanafamilia wao, na zinaweza kutumia Taifa ili kutoa maelezo (Kifungu cha 32 cha Itifaki ya Ziada ya I). Kanuni ya 117 ya Kanuni za CIHL inaashiria kwamba mgogoro vya vita vya silaha wa kimataifa na suio wa kimataifa wahusika kwenye mgogoro

Angalia, kwa mfano, Sheria ya Iraqi Namba 13 ya 2015, Sheria ya Maswala na Ulinzi na Makaburi ya Halaiki, kurekebisha Sheria Nambari 5 ya 2006, Ulinzi wa Makaburi ya Halaiki. 32 Kanuni ya 10(3) ya Kanuni za Kuongoza za 2019 kuhusiana na utafutaji wa watu waliopotea zinaamrisha ufikiaji bila kizuizi kwa mamlaka zinazofaa ikiwa ni pamoja na ‘mamlaka kamili ya kufanya ziara zisizotangazwa kwa kila mahali ambapo mtu aliyepotea anaweza kuwa, ikiwa ni pamoja na vituo vya kijeshi na polisi na majengo ya kibinafsi’. Pale inapohitajika, hii inapaswa kujumuisha ‘utunzaji wa eneo linalohusiana na utafutaji’ (ibid). 33 Kukhalashvili and others v Georgia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 8938/07 na 41891/07 (2 Aprili 2020) aya ya 129. 34 Ibid, katika aya ya 129. 35 Aslakhanova and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 2944/06 na 8300/07, 50184/07, 332/08, 42509/10 (18 Disemba 2012) yaa ya 230. 36 Da Silva v United Kingdom, Hukumu ya Baraza Kuu, Maombi ya ECtHR Nambari 5878/08 (30 Machi 2016) vifungu vya 231-238, inatoa muhtasari kamili wa Baraza Kuu wa mahitaji ya uchunguzi madhubuti. 37 The Massacres of El Mozote and other Places v El Salvador, Hukumu kuhusu Ustahili, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 252 (25 Oktoba 2012) aya ya 299. 38 Valle Jaramillo et al. v Colombia, Hukumu ya Ustahili, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 192 (27 Novemba 2008) aya ya 102. 39 Cyprus v Turkey, Hukumu ya Baraza Kuu, Maombi ya ECtHR Nambari 25781/91 (10 Mei 2001) aya ya 135. 40 Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Ripoti ya mtaalam huru ili kusasisha Seti ya Kanuni za kupambana na ukiukwaji (18 Februari 2005) Hati ya UN ya E/CN.4/2005/102/Add.1 (kwa kifupi Kanuni za Orentlicher) Kanuni ya 4. 31

9


‘lazima wachukue hatua zote zinazowezekana ili kuwajibika kwa watu walioripotiwa kupotea’. Miongozo ya 2019 ya uchunguzi wa uhalifu kutokana na ukiukaji wa sheria za kibinadamu41 inahitaji viwango vya uchunguzi kutii kanuni za uhuru na kutopendelea (Mwongozo wa 7); ukamilifu (Mwongozo wa 8); uharaka (Mwongozo wa 9) na uwazi (Mwongozo wa 10) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai inayohitaji wachunguzi ‘kuzingatia viwango vya juu zaidi vya uadilifu na mwenendo’.42 Uchunguzi wa makaburi ya halaiki unaweza kuunda sehemu muhimu ya uchunguzi mpana zaidi wa uwezekano wa vifo haramu. Maelezo kuhusu muktadha wa makaburi ya halaiki, yanayotolewa na mashahidi, wanajamii na manusura yanaweza kujumuisha maelezo muhimu kuhusu ulinzi na uchunguzi wa makaburi.43 Itifaki za Minnesota zinaainisha mahitaji ya chini yafuatayo kwa uchunguzi wa vifo vinavyoweza kuwa haramu: ‘(a) Kutambua waathiriwa (b) Kurejesha na kutunza vifaa vyote vinavyoweza kwa sababu ya kifo, utambulisho wa mhusika (wahusika) na hali zinazozunguka kifo; (c) Kutambua mashahidi wanaowezekana na kupata ushahidi wao kuhusiana na kifo na hali zinazohusiana na kifo; (d) Kubaini sababu, njia, mahali na wakati wa kifo, na hali zote zinazohusiana. (…) Na (e) Kubaini ni nani aliyehusika katika kifo na uwajibikaji wao binafsi kwa kifo hicho ‘(katika D.1.25. ukurasa wa 7, maelezo ya chini hayajajumuishwa). Masuala maalum ya kuzingatia katika utekelezaji bora wa uchunguzi wa kaburi la halaiki: Awamu ya kupanga (1) Kuzingatia mipango ya jumla • Ni huluki gani iliyo na jukumu la jumla kwa makaburi ya halaiki katika muktadha wa juhudi pana za watu waliopotea?44 • Nani anapaswa kupanga mchakato wa kufukua kaburi la halaiki, utambulisho na kurejesha mabaki ya binadamu? • Upeo wa uchunguzi uliopangwa ni upi? • Ni timu gani zenye taaluma mbalimbali zinahitaji kukusanyika na viwango vipi vya uwajibikaji?45 • Je, huluki mamlaka gani ya ziada inayoweza kuhusika na jinsi zitaratibiwa kwa pamoja? • Je, uchunguzi wa kaburi la halaiki unaendana vipi na shughuli zingine/pana za uchunguzi?46

(2) Mipango ya ufikiaji wa jamii na kupunguza athari mbaya • Uundaji wa mahusiano na uaminifu kupitia ufafanuzi unaozingatiwa wa madhumuni na michakato ya uchunguzi na usimamizi wa matarajio halisi ni muhimu. Hii itasaidia kupata ufikiaji wa eneo, muktadha, maelezo na kukubalika kwa vitendo. • Mipango inapaswa kutarajia na kutafuta kupunguza athari za jamii wakati huo huo ikidumisha uaminifu wa uchunguzi. (3) Mipango ya rasilimali, timu na ununuzi Bajeti na mpango wazi wa rasilimali zinazopatikana na zinazohitajika kwa uchunguzi inahitaji kukusanywa. Hii itajumuisha ukubwa na muundo wa timu itakayotumika, majukumu ya wafanyakazi (kuhakikisha mwendelezo inapowezekana) na awamu ya kuajiri.47 Uzingatiaji, panapofaa, inapaswa kutolewa kwa wachunguzi wa eneo (ikiwa ni pamoja na mahitaji ya mafunzo) uwezo wa muda mrefu. (4) Mipango ya usalama Usalama wa eneo pamoja na usalama wa kimwili na kisaikolojia wa wafanyakazi ni muhimu zaidi. Baadhi ya maeneo yanaweza kuwa hatari sana kwa uchimbaji48 au yasiyo salama kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. Usaidizi wa wataalam unaweza kuhitajika kuhusiana na hatari kama vile sumu, mabomu ya ardhini na vifaa vya kulipuka vilivyobuniwa (IED). Mbali na usalama wa eneo, uzingatiaji unapaswa kutolewa kwa usalama wakati wa usafirishaji wa wafanyakazi kwenda na kutoka kwa eneo na wakati wa kufanya kazi ya ushirikiano. (5) Mipango ya upeo, kiwango na mpangilio Upeo, pamoja na viashiria vya nyakati na vigezo, kwa uchunguzi utajumuisha kuzingatia kiwango na mpangilio wa uchimbuaji na uchambuzi wa makaburi ya halaiki. (6) Mipango ya Taratibu za Kawaida wa Uendeshaji na kuripoti Matumizi ya Taratibu za Kawaida za Uendeshaji, viwango vya ushahidi vinavyokubalika kwa jumla na itifaki za ushughulikiaji/utunzaji wa ushahidi na kurekodi itahakikisha ubora, uthabiti na uwazi wa michakato, na inahitaji kukubaliwa. Kwa kuongezea, mfumo wa kudhibiti ubora unapaswa kutayarishwa kwa ajili ya utekelezaji. (7) Mipango ya sababu za nje Uchafuzi, kuchanganyika na ‘uchimbaji’ wa mtu mwingine unaweza kuathiri awamu ya kupanga.

Geneva Academy na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) (2019), Miongozo ya kuchunguza ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu: sheria, sera, na mazoea mazuri. 42 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (2008), Kanuni za Maadili ya Wachunguzi, ICC/AI/2008/005 kifungu cha 4.1. 43 Itifaki ya Minnesota, kwa mfano, ina sehemu kuhusiana na Mahojiano na Ulinzi wa Mashahidi ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Kina kuhusu Mahojiano (katika sehemu ya V, B. kurasa za 33-35). 44 Hii itategemea mpangilio wa taasisi, mamlaka na majukumu. 45 Angalia Kiambatisho cha 2 kuhusu taaluma na wataalam ambao wanaweza kuwa sehemu ya timu. Kwa maelezo kuhusu majukumu ya usimamizi kama sehemu ya Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga angalia Kiambatisho cha 8: Wajibu wa Usimamizi wa DVI wa Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol. 46 Utoaji wa jumla wa utekelezaji wa uchunguzi kuhusiana na vifo visivyo halali unaweza kupatikana katika Itifaki ya Minnesota sehemu ya IV kuhusu utekelezaji wa uchunguzi (kwenye kurasa za 12-15). Miongozo zaidi kuhusu chunguzi wa eneo la uhalifu inaweza kupatikana ndani ya Itifaki za Minnesota kwenye sehemu ya V kurasa za 30-32. 47 Taratibu za kulinda uzoefu, utaalam na ustahiki unaofaa pamoja na mzunguko wa usambazaji inaweza kusaidia kuwa sehemu ya hii. 48 UNAMI na OHCHR (2018) Kuchunguza Ukatili: Makaburi ya halaiki katika eneo linalodhibitiwa na ISIL. 41

10


(8) Mipango ya ushugulikiaji, uhifadhi, udumishaji na ulinzi wa data Sambamba na upeo wa uchunguzi, ushughulikiaji (utumiaji na utupaji) wa sampuli za marejeleo, sampuli kutoka kwa sehemu za mwili na ushahidi husika, unapaswa kuanzishwa. Miundo wazi inahitaji kuwekwa kwa data yote, pamoja na uhifadhi, ulinzi na udumishaji wa data, kulingana na sheria za data za ndani za Taifa lakini pia ikitambua sheria za kimataifa.49 (9) Mipango ya michakato ya kurejesha mabaki ya binadamu na/au kuhifadhi baada ya kufukuliwa kwa mwili Kabla ya ufukuaji kuanza, kunapaswa kuwa na mkakati wazi wa michakato ya kurejesha mabaki ya binadamu na, iwapo kutotambuliwa, kuhifadhi kwa heshima au mipango ya mazishi. (10) Mipango ya mkakati wa mawasiliano (ikiwa ni pamoja na matumizi ya picha) na uratibu (10.1) Mawasiliano ya ndani, uratibu na mpango unaofaa wa utekelezaji. (10.2) Mawasiliano ya nje na uratibu kati ya timu ya uchunguzi na mamlaka ya mashtaka ya kimahakama; hasa pale juhudi za utambulisho cha binadamu ni tofauti na mashirika ya mashtaka vya kitaifa au kimataifa. (10.3) Mawasiliano ya nje na uratibu kati ya timu ya uchunguzi na waathiriwa, familia, jamii na afisa wa ushirikiano na vyombo vya habari. Mawasiliano ya mapema na yanayoendelea ni muhimu kwa ukuzaji wa usaidizi halali wa na kushiriki katika mchakato wa kufukua maiti. Hii itajumuisha uhakikisho upya kwamba mabaki ya mwili yatashughulikiwa kwa uangalifu, utu na heshima, na kuhifadhiwa salama. Hii pia ni muhimu kwa utambulisho na azimio la urejeshaji, na inasaidia kuaminiwa kwa sheria na kukubali matokeo ya kimahakama. Mawasiliano yote ya umma yanapaswa kuwa sahihi, yasiyo na utata, mara kwa mara na kwa wakati unaofaa. Yanapaswa kujumuisha maelezo kuhusu: • Mchakato wa kupata na kurudisha mabaki ya binadamu; • Kuwepo (na yaliyomo, inapofaa) wa itifaki/hatua za ulinzi na usiri; • Uthibitishaji wa kifo; • Upatikanaji wa usaidizi unaofaa wa kisaikolojia kwa familia; na • Inapaswa kutafuta kudhibiti matarajio.

Mbinu ya uchunguzi wa kisheria Sambamba na hatua za kupanga zilizo hapo juu, mbinu ya uchunguzi wa kisheria inahitaji yafuatayo: (1) Matumizi ya Taratibu za Kawaida za Uendeshaji Wakati wote na katika hatua zote, Taratibu za Kawaida za Uendeshaji50 zinapaswa kutumika. Hii italinda uadilifu wa uchunguzi (haswa kuhusiana na utambulisho wa waathiriwa, upataji na uhifadhi wa ushahidi wote unaohusika na utambulisho, sababu, njia, wakati, mahali pa kifo, kuhamishwa na usumbufu wa mabaki ya binadamu na vile vile utambulisho wa mhusika(wahusika)). (2) Matumizi ya mifumo ya kudhibiti ubora Mfumo wa kudhibiti ubora utahakikisha Taratibu zote za Kawaida za Uendeshaji zinafuatwa. (3) Matumizi ya mfumo unaofaa wa ushughulikiaji wa ushahidi, kurekodi, kuripoti na kuhifadhi Hii itajumuisha urejeshaji na usafirishaji unaofaa, salama na wenye utu wa mabaki ya binadamu, na hatua za kuzuia uchafuzi. Ushahidi wote (wa sababu, njia na wakati wa kifo, maelezo ya demografia, jumla ya watu pamoja na utambulisho) unapaswa kuhifadhiwa, kurekodiwa, kuchambuliwa kwa ustadi na kuripotiwa, wakati huo huo ukidumisha mfululizo wazi wa kumbukumbu kwa utambulisho na michakato ya uwajibikaji inayowezekana. (4) Matumizi ya mkakati wa mawasiliano Kuwezesha ushiriki madhubuti na uhamasishaji na ushirikiano wa kifamilia na, inapofaa, uratibu na waendesha mashtaka/taasisi za mahakama na vyombo vya habari.

Kama vile Azimio la Ulimwengu kuhusu Maadili ya Kibiolojia na Haki za Binadamu (UNESCO 2005), kuhusu utafiti katika dawa, sayansi za maisha na teknolojia husika, ikiwa ni pamoja na jeni; Azimio la Kimataifa kuhusu Data ya Jeni za Binadamu (UNESCO 2003), kuhusu ukusanyaji, uchakataji, matumizi na uhifadhi wa data na sampuli za jeni ya binadamu: Azimio la Ulimwengu kuhusu Jeni za Binadamu na Haki za Binadamu (UNESCO 1997), kuhusu utafiti, ushughulikiaji au utambuzi unaoathiri jeni za mtu binafsi; Mkataba wa Haki za Binadamu na Dawa za Kibiolojia, Mkataba wa Oviedo (Baraza la Ulaya 1995), kulinda utu na utambulisho wa wanadamu kuhusu biolojia, dawa, utafiti wa kibiolojia na upimaji wa jeni. Angalia pia aaBB Kuendeleza Uingizaji wa Damu na Tiba za Seli Duniani (2010), Miongozo ya Shughuli za Utambulisho wa DNA wa Vifo vya Halaiki kwa maelezo kuhusu ushughulikiaji katika muktadha wa juhudi za utambulisho (katika ukurasa wa 11). 50 Kama vile Itifaki za Minnesota na haswa Miongozo yake ya Kina kuhusu Uchimbaji wa Makaburi, katika sehemu ya C kurasa za 36-37. 49

11


D. Utambulisho Kanuni za kimataifa Kifungu cha 15 cha CED kinasema: ‘Washirika wa taifa watashirikiana pamoja na kupeana viwango vikubwa zaidi vya usaidizi kwa nia ya kusaidia waathiriwa wa upoteaji unaotokana na mamlaka, na katika kutafuta, kupata na kuachilia watu waliopotea na, iwapo kifo, kufukua na kuwatambua na kurudisha mabaki yao’ (mkazo umeongezwa). Maelezo pia yanahitaji kufahamishwa kwa watu walio na nia halali ya maelezo kama hayo, kama vile jamaa (ibid, Kifungu cha 18). Na kifungu cha 24(3) cha CED kinahitaji kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu. Mataifa yamo chini ya wajibu wa kutoa maelezo ya kumbukumbu kuhusu mtu aliyekufa51 na kutenga rasilimali muhimu kwa uchimbaji wa maeneo ya mazishi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, uhifadhi na utambuzi wa mabaki ya binadamu.52 Utoaji wa cheti cha kifo ni muhimu sana.53 Kwa kuongezea, katika kesi ya Pueblo Bello Massacre v Colombia Mahakama ya Kimarekani ilipendekeza kuwa Taifa linapaswa kuhimiza umma kujitokeza na maelezo ambayo inaweza kusaidia kuwatambua waathiriwa.54 Thamani ya uchambuzi wa DNA kama njia ya msingi ya utambulisho inatambuliwa (Kanuni za ICMP Paris, Kanuni ya 6).55 Sheria ya kitamaduni ya kibinadamu ya kimataifa inaeleza kwamba wahusika kwenye mgogoro (iwe wa kimataifa au sio wa kimataifa) warudishe mabaki ya wafu baada ya kuombwa (Kanuni ya 114 ya CIHL) Kwa kuongezea, ‘[k]ila mshirika kwenye mgogoro lazima achukue hatua zote zinazowezekana kuwajibikia watu waliopotea kutokana na vita na anapaswa kuwapa wanafamilia wao maelezo yoyote inayohusu hatima yao’ (CIHL Kanuni ya 117). ICRC inapanua nafasi hii: ‘Mara tu hatima ya mtu aliyepotea inapobainishwa kuwa kifo, njia zote zinazopatikana lazima zifanyike ili kuhakikisha urejeshaji wa mwili na vifaa vyovyote vya kibinafsi’ (Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea, Kifungu 19). Sheria pia zinahusu mazishi

yanayotakiwa, ufukuaji na mazoea ya ukumbusho na jinsi ya kushughulikia mabaki ya binadamu ambayo hayajatambuliwa, zikiomba rekodi zihifadhiwe, juhudi za utambulisho ziendelee na familia ijulishwe. Ingawa utambulisho unaunda sehemu muhimu ya uchunguzi na utambuzi wa haki, inaeleweka kama jukumu la njia.56 Utambulisho wa mabaki ya binadamu ni sharti la kurudishwa kwa mabaki kwa familia ili kuwezesha mazoea ya ukumbusho lakini pia kwa familia kupokea cheti cha kifo.57 Mahitaji ya ndani ya eneo: Urejeshaji, kurekodi na kuhifadhi mabaki ya binadamu na ushahidi husika unapaswa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika sehemu ya uchunguzi. Jitihada za nje ya eneo: Uchunguzi wa baada ya kufa58 na ushahidi husika unafanywa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Kazi kama hii kwa kawaida inahitaji upangaji mahususi na utengaji wa rasilimali zaidi. Kwa kuongeza, yafuatayo yanahitajika: • Udumishaji wa mfululizo wazi wa kumbukumbu wa michakato ya utambulisho na uwajibikaji; • Vifaa vya kutosha vya uhifadhi na udumishaji wa mabaki ya binadamu; na • Uwezo wa familia zinazotembelea chumba cha kuhifadhi maiti wa kutambua na/au kuona ushahidi husika. Ukusanyaji wa data ya watu waliopotea ikiwa ni pamoja na sampuli za marejeleo ya DNA ya familia zinahitajika kutoa maelezo ili kuwezesha utambulisho. Data hii lazima ikusanywe kwa njia nyeti ambayo inalinda haki za manusura na marehemu. Mazoea kama haya yanayohusiana na data ya kibinafsi, maelezo ya jeni na uhifadhi wa maelezo kama hayo lazima yazingatie sheria za ndani za data na yatambue viwango vya kimataifa.

The Massacres of El Mozote and other Places v El Salvador, Hukumu kuhusu Ustahili, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 252 (25 Oktoba 2012) aya ya 334. 52 Aslakhanova and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 2944/06 na 8300/07, 50184/07, 332/08, 42509/10 (18 Disemba 2012) yaa ya 226. 53 Utoaji na uchakataji wa vyeti vya kifo ulikuwa kiini cha Mkataba wa UN kuhusu Azimio la Vifo vya Watu Waliopotea baada ya Vita vya Kidunia vya II (1939-1945) ambalo lilitumika hadi 1972. Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Kupotea inaelezea katika muhtasari wake wa Kifungu cha 4 ‘Katika tukio la kifo, kuna jukumu la kutoa cheti cha kifo, kushughulikia mabaki ya binadamu kwa heshima na utu, na vile vile kurudisha mwili kwa familia na/au kuhakikisha mazishi’ (katika ukurasa wa 12) na yanapaswa kufanywa na mamlaka adilifu (katika ukurasa wa 44). Zaidi ya hayo, vyeti vya kifo vinatambuliwa katika Usimamizi wa Miili ya Wafu baada ya Majanga wa ICRC: Mwongozo wa Eneo la Kazi kwa Wahudumu wa Kwanza, kwa mfano, kwenye ukurasa wa 30; na Utambulisho cha Waathirika wa Majanga wa Interpol, katika 5.4. Awamu ya 4: Upatanisho, kwenye ukurasa wa 17. 54 Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 272. 55 Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea (2019), Kanuni za ICMP Paris, Toleo Lililofafanuliwa, ICMP.DG.468.1.W.doc. 56 Ingawa Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol unaonyesha mbinu mahususi zaidi kupitia kusema: ‘Waathiriwa wana haki ya utambulisho baada ya kifo chao’ (Sehemu ya B, Kiambatisho cha 2, Ripoti Rasmi - DVI). 57 Hali maalum ni kwa sheria ya Ajentina Nambari 14,321 ya 11 Mei 1994 ambayo inaunda aina ya waliotoweka kwa nguvu kama sawa kisheria na kifo kwa madhumuni ya raia. Inaruhusu familia kushughulikia wosia, kushughulikia mali ya vitu vya aliyepotea na maswala ya urithi, lakini uwezekano wa ‘kupatikana tena’ kwa mtu huyo unabaki wazi. Azimio kama hilo kwa linakubali kwa uwazi kuhusika kwa Taifa au jukumu la kifo cha mtu huyo (tofauti na cheti cha kifo tu). 58 Kwa mfano, kulingana na Miongozo ya Minnesota kuhusu Uchunguzi wa Baada ya Kifo inayotoa mwongozo kuhusu uchunguzi wa maiti, uchunguzi wa meno na uchambuzi wa anthropolojia wa mabaki ya mifupa, kama ilivyo kwenye Mwongozo wa E kwenye kurasa za 49-51 na vile vile Viambatisho vya 1-5, kurasa za 57-87 zinazotoa kanuni. Hizi zinaweza kufanyika katika vituo salama vya muda vya kuhifadhi maiti. 51

12


Mfumo wa usimamizi wa data unaolingana na nyanja zote za ukusanyaji na uchambuzi wa data pia ni hitaji ya nje ya eneo ili kuwezesha utambulisho. Kama kiwango cha chini, hii itajumuisha: • Usajili wa watu waliopotea na maelezo husika; • Maelezo ikiwa ni pamoja na sampuli za marejeleo ya DNA ya familia za waliopotea; • Data kuhusu shughuli za uchunguzi wa akiolojia na urejesho wa mabaki ya binadamu na ushahidi husika; • Uchunguzi wa anthropolojia na orodha ya kesi; • Michakato ya maabara ya DNA; • Hifadhidata ya wasifu wa DNA; na • Kulinganisha DNA. Uwezo wa kuchakata DNA hauhitaji kuwepo nchini kwa sababu unaweza kupatikana kupitia mashirika ya watu wengine yanayoweza kutoa usaidizi wa upimaji wa DNA kwa kiwango kikubwa. Mkakati wa mawasiliano utawezesha: • Ufafanuzi wa michakato na wakati wa utambulisho na uchakataji wa data kwa wanafamilia na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kukubalika; • Kuzijulisha familia kuhusu maamuzi kuhusiana na uchunguzi wa baada ya kufa, na matokeo ya uchunguzi kama huo. Hii inapaswa kujumuisha maelezo kuhusu usaidizi wa familia na chaguo za rufaa; • Mawasiliano bora na mashirika ambayo yanaweza kuhifadhi na kutoa maelezo ya ziada; • Mawasiliano bora na vyombo vya habari ambayo inaheshimu haki za faragha za familia zilizoathiriwa, hutambua unyeti wa familia na haki ya kujua matokeo kabla ya mawasiliano na vyombo vya habari. Matokeo yanayowezekana ya juhudi za utambulisho (1) Utambulisho chanya: inagundulika ambapo kuna udhabiti kati ya data ya mtu aliyepotea na kabla ya kufa na baada ya kufa na hakuna tofauti ambazo haziwezi kuelezewa. Mbinu za utambulisho za kuaminika za kisayansi ikiwa ni pamoja na alama za vidole, uchunguzi wa meno, wasifu wa kibaolojia kupitia uchunguzi wa anthropolojia ambapo mabaki yanapangwa kwa mifupa, na uchambuzi wa DNA unapaswa kutumika. Utambuzi wa kuona (ikiwa ni pamoja na picha), maelezo ya kibinafsi, tatoo, mali na mavazi yanayopatikana mwilini na vile vile matokeo ya kimatibabu yanaweza kusaidia utambulisho lakini hayapaswi kutumika kama kitambulishi pekee.59 Ambapo utambulisho umebainika, mamlaka inayofaa inapaswa kutoa cheti cha kifo60.

(2) Utambulisho haujabainika: ambapo, kwa mfano, ushahidi unaunga mkono kutengwa kwa nadharia fulani kuhusu utambulisho wa mabaki ya binadamu, au ambapo hakuna hitimisho kuhusu utambulisho wa mabaki ya binadamu.61 Rekodi inapaswa kuhifadhiwa kikamilifu ili kuruhusu utambulisho wa baadaye na arifa inayofuata kwa jamaa na wahusika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya serikali. Udumishaji na hatua za uhifadhi wa muda mrefu zinahitajika kulinda matarajio ya utambulisho cha baadaye. Ambapo hatua za udumishaji na uhifadhi hazipatikani au hazifai, mabaki ya binadamu ambayo hayajatambuliwa yanaweza kuzikwa katika makaburi yaliyotiwa alama kulingana na mila na desturi zinazofaa za kidini za marehemu.62 Ili kuhakikisha uwezekano wa utambulisho wa baadaye, uteketezaji wa mwili unapaswa kuepukwa kila inapowezekana. Ufuatiliaji wa mabaki unapaswa kuhakikishwa kupitia mbinu kama vile: • Uwekaji wa kumbukumbu na kuambatisha eneo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha eneo la miili ya kibinafsi ndani ya eneo; • Kuweka nambari na alama kwa kila mwili na mfuko/ jeneza kwa kurejelea nambari ya sampuli ya DNA na uhifadhi; • Matumizi ya ishara ili kuweka alama kwenye eneo; • Uhifadhi salama wa maelezo ili kuhakikisha usalama wake. (3) Utambulisha usio sahihi: ambapo kuna hitilafu katika kutoa utambulisho kwa mabaki ya binadamu. Utambulisho kama huo usio sahihi utakuwa na athari mbaya kwa seti mbili za familia zinazohusika na vile vile uchunguzi. Ugunduzi wa hililafu kama hiyo unapaswa kuchochea ushirikiano unaofaa na usaidizi wa kifamilia na vile vile hatua ya kurekebisha kulingana na Taratibu za Kawaida za Uendeshaji. Haki za familia katika kisa cha kutotambuliwa Katika hali ya kutotambuliwa, wanafamilia waliobaki hata hivyo wanaweza kuhitaji baadhi ya vyeti ili kuthibitisha kutokuwepo kwa wapendwa wao na kuwawezesha kudai haki zingine au kuendelea na uuzaji wa mali, urithi, kuoa tena n.k. Hali au cheti kisichokuwepo kinapaswa kutolewa ili kulinda haki za familia.63

Angalia Mbinu za Utambulisho (Msingi na za Pili) kama sehemu ya Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol kwenye ukurasa wa 18; Mwongozo wa Utambulisho cha Waathiriwa wa Majanga wa Interpol Kiambatisho cha 12 kuhusu Mbinu za Utambulisho na Itifaki ya Minnesota, sehemu ya E kuhusu Utambulishi wa Miili iliyokufa, kurasa za 21-24. 60 Kama, kwa mfano, Cheti cha mfano cha kifo katika Kiambatisho 2 cha ICRC/Sheria ya Mfano kuhusu Waliopotea. 61 Angalia Itifaki ya Minnesota, sehemu E kuhusu Utambulisho wa Miili iliyokufa, ukurasa wa 24. 62 Mazishi kama hayo ya mabaki ambayo hayajadaiwa na ambayo haijatambuliwa yanachukuliwa kuwa sahihi na Azimio la Mytilini linalohusika na utunzaji wa heshima wa watu waliopotea na waliokufa na familia zao kama matokeo ya safari za wahamiaji (Azimio la Mytilini la Utunzaji wa Utunzaji wa Heshima wa Watu Wote Waliopotea na Waliokufa na Familia zao kama Matokeo ya Safari za Wahamiaji (2018) katika Kifungu cha 16). Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea katika ufafanuzi wake wa Kifungu cha 22 (Mazishi na ufukuaji wa maiti) inasema ‘[u]teketaji unapaswa kuepukwa, isipokuwa pale inapobidi (kwa mfano kwa sababu ya afya ya umma) na rekodi ya sababu hio kuhifadhiwa, ikiwa ni pamoja na majivu’ (katika ukurasa wa 48). 63 Sawa na aina ya Watu Waliopotea katika Ajentina na Sheria ya Kolombia ya 1531 kuhusu Azimio la Kutokuwepo kwa Watu Waliopotea, 2012, Kifungu cha 7. Chini ya sheria za kimataifa hali ya kisheria ya mtu aliyepotea na jamaa zao haidhibitiwi lakini CED inatoa katika Kifungu cha 24(6) ‘Bila kuathiri jukumu la kuendelea na uchunguzi hadi hatima ya mtu aliyepotea itakapofafanuliwa, kila Mshirika wa Taifa atachukua hatua stahiki kwa kuzingatia hali ya kisheria ya watu waliopotea ambao hatima yao haijafafanuliwa na ile ya jamaa zao, katika nyanja kama vile ustawi wa jamii, maswala ya kifedha, sheria ya familia na haki za mali.‘ 59

13


E. Kurudishwa kwa mabaki ya binadamu Kanuni za kimataifa Kifungu cha 24(3) cha CED kinasisitiza wajibu wa kurudisha mabaki ya binadamu waliopotea kwa wanafamilia walio hai; na kifungu cha 15 kinachohitaji Mataifa kutoa ushirikiano na usaidizi katika juhudi zao za kutafuta na kurudishwa. Kanuni ya 2(4) ya Kanuni za Kuongoza za 2019 inabainisha kuwa ‘kurudishwa [kwa mabaki ya binadamu] kunapaswa pia kuhusisha njia na taratibu zinazohitajika kuhakikisha mazishi yenye heshima yanayolingana na matakwa na mila ya kitamaduni ya familia na jamii zao.’ Hili linaweza kujumuisha kugharamia ada za uhamishaji kati ya mipaka wa mabaki ya binadamu. Maarifa ya sheria kutoka kwa Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu inasema: ‘Wakati mabaki ya mwili yanapatikana na kutambuliwa, Taifa lazima iyarudishe kwa jamaa zake haraka iwezekanavyo, baada ya kudhibitisha uhusiano wa jeni, ili aweze kuheshimiwa kulingana na kanuni zake. Taifa pia inapaswa kulipia gharama za mazishi, kwa makubaliano na jamaa wa karibu.’64 Kutorejeshwa kwa mabaki ya binadamu na mazishi katika maeneo ambayo hayajabainishwa kutakuwa ukiukaji wa haki ya familia na maisha ya kibinafsi; uingiliaji ambao unaruhusiwa tu panapokubaliwa na sheria, ni kutafuta lengo halali (kama vile usalama wa umma, kuzuia machafuko au haki na uhuru wa wengine) na kunahitajika katika jamii ya kidemokrasia.65 Katika sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ‘kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kwa ombi na mshirika au ndugu wa karibu, kama ishara ya kuheshimu maisha ya familia na kuhusiana na haki za mwathiriwa, inatumika wakati wa vita vya kimataifa na visivyo vya kimataifa’ (CIHL, Kanuni ya 114). Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Kifungu cha 21(4) cha Waliopotea inasema kwamba ‘[m]abaki ya binadamu na vifaa vya kibinafsi zitarejeshwa kwa familia’.

Baada ya kukamilisha michakato ya uchunguzi, utambulisho na haki, mabaki ya binadamu, sehemu husika za mwili na vifaa vya kibinafsi zinapaswa kurudishwa kwa wanafamilia, na kuwaruhusu kuzika marehemu kulingana na imani zao.

Ambapo utambulisho na kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kunawezekana: • Baada ya uchunguzi wa baada ya kufa, mabaki yanapaswa kutolewa kwa familia mapema iwezekanavyo. • Mchakato wa kurudisha mabaki ya binadamu unapaswa kutekelezwa na kufuatwa. Inapaswa kujumuisha mkakati unaofaa wa mawasiliano, na, inapowezekana, pendekezo la, au rufaa, rasilimali kwa usaidizi kwa familia na jamii zilizofiwa. Ambapo mwili umetambuliwa lakini haujadaiwa na mwanafamilia: • Mabaki ya binadamu na rekodi zote husika zinaweza kuhifadhiwa/kudumishwa; AU • Mabaki ya binadamu yanaweza kuzikwa katika makaburi yaliyotiwa alama kulingana na mila ya kitamaduni au mila mwafaka za kidini za marehemu na rekodi husika zinaweza kuhifadhiwa. Kwa chaguo lolote linalopendelewa, mipango inapaswa kujumuisha utoaji wa uhifadhi unaoweza ufuatiliaji, wa muda mrefu au uzikaji wa maiti. Mipango inapaswa kufaa utamaduni, na uzingatiaji inapaswa kutolewa kwa mahali mpya pa kuzikwa kama eneo lenye umuhimu na ukumbusho kwa familia na jamii. Hali za ziada zitajumuisha maswala ya umiliki wa ardhi, hali iliyopo ya udongo na urefu wa meza ya maji ya chini ya ardhi katika eneo lililokusudiwa. Kama ilivyo kwa miili ambayo haijatambuliwa (angalia hapo juu, kifungu cha D kuhusu utambulisho), na kuwezesha urekebishaji wa utambulisho wa kimakosa na kurudishwa kwa kimakosa kwa mabaki ya binadamu, ufuatiliaji unapaswa kuhakikishwa kupitia mbinu kama vile: • Uwekaji wa kumbukumbu na kuambatisha eneo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha eneo la miili ya kibinafsi ndani ya eneo; • Kuweka nambari na alama kwa kila mwili na mfuko/ jeneza kwa kurejelea nambari ya sampuli ya DNA na uhifadhi; • Matumizi ya ishara kuweka alama kwenye eneo; na • Uhifadhi salama wa maelezo ili kuhakikisha usalama wake. Kutekekeza maiti kunapaswa kuepukwa. Viungo husika vya mwili na ushahidi Njia zinazofaa kitamaduni za kushughulikia vifaa binafsi ambavyo havijadaiwa na sehemu za mwili ambazo hazijatambuliwa au hazijadaiwa zinapaswa kukubaliwa na jamii zilizoathiriwa.66 Hii inaweza kujumuisha ukumbusho, maonyesho nyeti, mazishi, maeneo maalum ya ukumbusho au mahali pa uhifadhi wa mifupa ya wafu.

Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 273. 65 Sabanchiyeva and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 38450/05 (6 Juni 2013) aya za 117-134. 66 Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Maafa ya Majanga wa Interpol, Kiambatisho cha 17: Jukumu na Wajibu wa Mwanaanthropolojia wa DVI unapendekeza ‘ukaguzi wa mwisho wa uchunguzi wa kisheria wa anthropolojia na kukagua mabaki ya mwili katika matukio yaliyo na mabaki yaliyogawanyika na/au yaliyobadilishwa. Kabla ya kutolewa kwa mabaki kwa ndugu wa karibu, ukaguzi wa mwisho ya anthropolojia unaongeza safu ya ziada ya uhakikisho wa ubora na udhibiti ambao unadumisha kiwango cha juu cha uaminifu na familia za waathiriwa’ (katika ukurasa wa 3). 64

14


F. Haki Kanuni za kimataifa a. Utoaji wa maelezo: Haki ya ukweli imejikita katika Vifungu vya 32 na 33 vya Itifaki I ya Ziada ya Mikataba ya Geneva, iliyojumuishwa katika mkutano wa haki za binadamu (Dibaji ya CED na Kifungu cha 24 (2)), maarifa ya sheria67 na kufafanuliwa katika sheria zisizoshurutisha. Haki inajumuisha hitaji la waathiriwa, familia na jamii ya kujua ukweli kuhusu matukio ya zamani, ikiwa ni pamoja na hali na sababu ambazo zilisababisha kutekelezwa kwa uhalifu huo (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 2). Katika kisa cha kifo au upoteaji unaotokana na mamlaka, haki ya ukweli ni pamoja na haki ya familia kujua hatima na mahali walipo wapendwa wao. Ujifunzaji na maarifa ya majii pia yanajumuisha jukumu kwa Taifa kuhifadhi kumbukumbu ya pamoja ya tukio (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 3). b. Suluhisho: Kwa waathiriwa na familia zao, sheria za kimataifa kupitia Kanuni na Miongozo ya Msingi ya 2005 na CED (kwenye Vifungu vya 24(4) na 24(5)) hutoa suluhisho kadhaa zinazowezekana: • Fidia; • Marejesho; • Urekebishaji; • Kuridhika (ikiwa ni pamoja na uthibitisho wa ukweli na/au utafutaji, urejeshaji, utambulisho na mazishi) na; • Dhamana za kutorudia (kupitia, kwa mfano, kanuni za maadili, elimu na mafunzo).68 Katika kutafuta suluhisho69 waathiriwa wana haki ya: • Ufikiaji sawa na fanisi wa haki; • Fidia ya kutosha, inayofaa na ya haraka kwa madhara yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa kisaikolojia kwa jamaa wa karibu70; na • Ufikiaji wa maelezo muhimu kuhusu ukiukaji na mbinu za kufidia.

Hii imepata kuelezwa katika kisa cha mauaji ya Mapiripán: ‘wakati wa michakato ya uchunguzi na kimahakama, waathiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu, au ndugu zao wa karibu, wanapaswa kuwa na fursa za kutosha kushiriki na kusikilizwa, zote kuhusiana na ufafanuzi wa ukweli na adhabu ya wale waliohusika, na katika kutafuta fidia ya haki’.71 c. Katazo na adhabu au uhamishaji: Mauaji ya halaiki, ukiukaji mkubwa wa Mikataba ya Geneva, mateso na upoteaji unaotokana na mamlaka umepigwa marufuku na mkataba, na Washirika wa Mataifa wanahitajika kutunga sheria ya ndani ili kutoa adhabu madhubuti pale ambapo ukiukwaji unatokea (tazama Kifungu cha 5 cha Mkataba wa Mauaji ya Halaiki; Kifungu cha 49 cha GC I; Kifungu cha 50 cha GC II; Kifungu cha 129 cha GC III; Kifungu cha 146 cha GC IV; Kifungu cha 2 na 4 cha UNCAT; Kifungu cha 6 cha CED; na Kifungu cha 6 cha ICCPR kuhusiana na mauaji ya halaiki). Kufuatia kunyimwa kwa haki ya kuishi, jukumu la kuchunguza linajumuisha ‘utambulisho na, ikiwa inafaa, adhabu ya wale waliohusika’.72 Kanuni za Kuongoza za CED zinabainisha kuwa ‘utafutaji wa mtu aliyepotea na uchunguzi wa jinai wa watu wanaohusika na kutoweka kunapaswa kuimarishana ‘(Kanuni ya 13(1)). Mikataba ya Geneva inahitaji Washirika wa Mataifa kuwatafuta kikamilifu wahusika wanaodaiwa ili wawafikishe mahakamani kwa mashataka (Kifungu cha 49 cha GC I; Kifungu cha 50 cha GC II; Kifungu cha 129 cha GC III; Kifungu cha 146 cha GC IV). d. Utangazaji rasmi: Sambamba na haki za ziada za waathiriwa, kama matarajio ya haki ya jamii ya kidemokrasia na kama hatua ya kuimarisha heshima kwa sheria, matokeo ya uchunguzi wowote yanapaswa kutangazwa rasmi kikamilifu.73 Ugunduzi na uchunguzi wa eneo la kaburi la halaiki unaweza kutokea ndani ya muktadha mpana wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Katika hali kama hizo, mahitaji ya haki ya watu binafsi, jamii, Mataifa na jamii ya kimataifa yanaweza kuwa ya kuongezeka na ya kupingana. hitaji la na/au haki ya urekebishaji wa pamoja na upataji nafuu, uwajibikaji, mshikamano wa jamii, uaminifu na upatanisho.

Kwa uamuzi wa mapema angalia Velásquez Rodríguez v Honduras, Hukumu kuhusu Ustahiki, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu C Nambari 4 (29 Julai 1988), aya ya 177. Haki ya ukweli inahitaji uchunguzi wenye mamlaka juu ya unyanyasaji wa haki za binadamu pamoja na muktadha wa kijamii na kisiasa unaosababisha unyanyasaji; unajumuisha hatua ya ushiriki wa waathiriwa katika mchakato na utangazaji rasmi wa matokeo ya uchunguzi ili kufaidi jamii na mtu binafsi. 68 Kama ilivyoainishwa katika UNGA, Kanuni na Miongozo ya Msingi kuhusu Haki ya Suluhisho na Malipo kwa Waathiriwa wa Ukiukaji Mkubwa wa Sheria za Kimataifa za Haki za Binadamu na Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, Kanuni za 19-23. 69 Kanuni za Msingi, Kanuni ya 11. 70 Pueblo Bello Massacre v Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 274. 71 Mapiripán Massacre v Colombia, Hukumu ya Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 134 (15 Septemba 2005), aya ya 219. 72 Kukhalashvili and others v Georgia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 8938/07 na 41891/07 (2 Mei 2020), aya ya 129. Angalia pia Pueblo Bello Massacre v Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya za 265-269 kuhusu wajibu wa Taifa katika kuchunguza ukweli wa kesi na, inapobidi, kutambua, kushtaki na kuadhibisha waliohusika. 73 ‘Las Dos Erres’ Massacre v Guatemala, Hukumu ya Mapingamizi ya Awali, Ustahiki, Malipo na Gharama, IACtHR Mfululizo wa C Nambari 211 (24 Novemba 2009) vifungu vya 256-264 na El-Masri v the Former Yugloslav Republic of Macedonia,Hukumu ya Baraza Kuu la Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 39630/09 (13 Disemba 2012), aya ya 192 na Maoni ya Pamoja ya Maamuzi ya Majaji Tulkens, Spielmann, Sicilianos na Keller. 67

15


(1) Utoaji wa maelezo: Kujua kile kilichotokea kupitia michakato ya uchunguzi ni sharti la utambuzi wa mahitaji ya haki. Uchunguzi kaburi la halaiki na ufukuaji wa maiti, kupitia maelezo wanayofichua, unaweza kuchangia kufanikiwa kwa ukweli na kuwa utangulizi wa malengo ya haki katika viwango kadhaa. Hasa, matokeo ya uchunguzi wa kaburi la halaiki na kumbukumbu zinaweza kusaidia katika kutoa: • Maelezo kuhusu matukio yaliyosababisha unyanyasaji wa haki za binadamu; • Kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kwa madhumuni ya ukumbusho, na kutolewa kwa hati ya kifo (au hati inayolingana) ili kulinda hali ya kiuchumi wa familia, ikiwa ni pamoja na elimu na mahitaji ya kiafya; • Kutambuliwa kwa mwathiriwa na vile vile manusura; na • Kutambuliwa kwa wahusika. (2) Suluhisho: Kutoka kwa maelezo haya, haki zingine, haki za kufidiwa na madai ya kisheria yanaweza kufikiwa kwa: • Kuwezesha fidia, ikiwa ni pamoja na utambuzi rasmi, fidia, kuridhika na ukumbusho; • Kuwasilisha maombi chini ya masharti ya haki za binadamu ya ndani, kikanda na/au kimataifa; na • Kuwezesha mashtaka ya jinai. (3) Katazo na adhabu au uhamishaji: Uchunguzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi wa uhalifu unaolenga uwajibikaji wa wahusika unapaswa kuimarishwa, na njia wazi za mawasiliano na waendesha mashtaka/mamlaka za mahakama ni muhimu. Thamani fulani ya uchunguzi wa kaburi la halaiki kwa michakato ya kimahakama inaweza kujumuisha: • Uthibitisho wa kumbukumbu ya mashahidi; • Idadi ya vifo; • Sababu, njia na tarehe/wakati wa kifo; • Jinsia, umri na kabila la waathiriwa; • Utambulisho wa waathiriwa; • Jaribio za kuficha uhalifu kwa kuhamisha miili kutoka makaburi ya msingi hadi ya makaburi ya pili; na • Muunganisho dhahiri na wahusika.74 Kukamilika kwa uchunguzi wowote wa kimahakama na mchakato wa mashtaka haipaswi kuathiri vibaya mwendelezo wa uchunguzi wa kaburi la halaiki na juhudi za ulinzi. (4) Kwa juhudi za Taifa zinazolenga haki na uwajibikaji, kuripoti kwa uhuru na mamlaka kuhusiana na matokeo ya uchunguzi, kama sehemu muhimu ya mchakato wa uchunguzi, inaweza kuchangia kutimiza haki ya mwathiriwa ya kujua nini kilitokea, kumbukumbu ya pamoja na usaidizi kwa Sheria. Matokeo ya uchunguzi

wa kaburi la halaiki kwa hivyo yanapaswa kuripotiwa hadharani, isipokuwa kufanya hivyo itaathiri au kuhatarisha mashtaka ya jinai yanayoendelea au ya baadaye.

G. Ukumbusho Kanuni za kimataifa Haki ya kuzika wanafamilia kwa ujumla inaangaziwa kupitia ulinzi wa maisha ya kibinafsi na ya familia.75 Njia ya kuzika wafu inaweza kuunda jambo muhimu la mazoea ya kidini yanayolindwa chini ya uhuru wa mawazo, dhamiri na sheria za dini.76 Aidha, kuunda kumbukumbu kuhusu marehemu inaweza kuunda sehemu a dhamana ya juhudi za kutorudia.77 Kanuni za Orentlicher zinahitaji kwamba Taifa zihifadhi kumbukumbu ya pamoja ya matukio (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 3).78 Kanuni ya 115 ya CIHL inasema kwamba ‘wafu lazima wazikwe kwa njia ya heshima na makaburi yao yaheshimiwe na kuhifadhiwa vizuri’. Makaburi ya halaiki yanaweza kuwa matata, yenye changamoto na/au ya kutatanisha katika mazingira ya kijamii, kisiasa na kijiografia. Wakati wa kuchunguzwa na kuchimbwa, makaburi yote ya zamani ya halaiki na sehemu mpya za mazishi na ukumbusho zinaweza kuwa maeneo ya ukumbusho binafsi na/au pamoja; maonyesho ya mazoea ya kitamaduni, dini na siasa; na kuunda sehemu ya fidia. Kwa hivyo makaburi mengi yanaweza kuwa vyanzo vya: • Kuendeleza kumbukumbu ya kihistoria; • Kuchangia kwenye mazungumzo ya kitaifa kuhusu matukio ya zamani; • Mifumo ya usaidizi wa kisaikolojia na kijamii; • Kuathiri sera za baadaye; na/au • Kuwezesha hali ya msingi ya jamii yenye haki. Makaburi ya halaiki yaliyochimbiwa yanaweza kuhitaji utambuzi na ulinzi wa kisheria kama maeneo ya ukumbusho. Maeneo ya makaburi ya halaiki ambayo hayawezi kuchunguzwa pia yanaweza kuwa mahali pa ukumbusho na yanapaswa kutambuliwa kisheria na kulindwa kwa kiwango kinachowezekana ili kuhakikisha uadilifu wa ushahidi ikiwa kuna uwezekano wa uchunguzi utakaokea baadaye.

Kama ilivyotolewa kutoka kwa uzoefu wa ICTY na kesi kama vile Prosecutor v Mladić, Hukumu, IT-09-02-T-117281 (22 Novemba 2017) na Prosecutor v Karadžić, Toleo la Hukumu la Umma lililohaririwa na kutolewa mnamo 25 Machi 2016, IT-95-5 / 18-T (25 Machi 2016). 75 Kama ilivyoonyeshwa, kwa mfano, katika Sabanchiyeva and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 38450/05 (6 Juni 2013) 76 Johannische Kirche & Peters v Germany, Uamuzi, Maombi ya ECtHR No 41754/98 (10 Julai 2001). 77 Kwa mfano, ‘Las Dos Erres’ Massacre v Guatemala, Hukumu ya Mapingamizi ya Awali, Ustahiki, Malipo na Gharama, IACtHR Mfululizo wa C Nambari 211 (24 Novemba 2009), aya ya 265 na Pueblo Bello Massacre v Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 278. 78 Uzingatiaji wa uhuru wa haki za kujieleza unaweza kutokea katika muktadha wa ukumbusho kama huo au maeneo ya mauaji kama ilivyoonyeshwa katika Faber v Hungary, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 40721/08 (24 Julai 2012) ambapo Mahakama inakubali ‘kwamba onyesho la ishara isiyo wazi katika maeneo mahususi ya mauaji ya halaiki yanaweza katika hali fulani kuelezea utambulisho na wahusika wa uhalifu huo; ni kwa sababu hii kwamba hata ujielezaji uliolindwa vinginevyo hauruhusiwi sawa katika sehemu zote na nyakati zote’ (katika aya ya 58). 74

16


Kiambatisho cha 1 Miongozo muhimu, kanuni, mwongozo, mwongozo wa mazoea mazuri na itifaki: • aaBB Kuendeleza Uhamisho na Damu na Tiba ya Seli Ulimwenguni Kote (2010), Miongozo ya Uendeshaji wa Utambulisho wa DNA wa Vifo vya Halaiki www.aabb.org/ programs/disasterresponse/Documents/ aabbdnamassfatalityguidelines.pdf • Baraza la Ulaya (2011), Mkataba wa kuzuia na kupambana na unyanyasaji dhid ya wanawake na unyanyasaji wa nyumbani, CETS 210 11.V.2011 www.coe.int/en/web/conventions/full-list/-/ conventions/treaty/210 • Cox, M et al. (eds) (2008), The Scientific Investigation of Mass Graves: Towards Protocols and Standard Operating Procedures (Cambridge University Press) • Shule ya Folke Bernadotte Academy na Chuo cha Ulinzi cha Kitaifa cha Uswidi (2011), Mwongozo wa kusaidia katika uchunguzi wa jinai wa kimataifa https://fba.se/ contentassets/6f4962727ea34af5940fa8c448f3d 30f/handbook-on-assisting-internationalcriminal-investigations.pdf • Shule ya Geneva Academy na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) (2019), Miongozo kuhusu uchunguzi wa ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu: sheria, sera, na mazoea mazuri www.icrc.org/en/document/guidelinesinvestigating-violations-ihl-law-policy-and-goodpractice • Utiifu wa Haki za Ulimwenguni (2016), Viwango vya Msingi vya Uchunguzi kwa Wahudumu wa Kwanza kwa Uhalifu wa Kimataifa www.globalrightscompliance.com/en/ publications/basic-investigative-standards-forinternational-crimes • Chama cha Mawakili cha Kimataifa: Mwongozo wa Taasisi ya Haki za Binadamu (2009) kuhusu Ziara za Kimataifa za Kupata Haki za Binadamu na Ripoti (“Miongozo ya Lund-London”) www.ibanet.org/Fact_Finding_Guidelines.aspx • Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea (ICMP) (2018), Miongozo ya Wahudumu wa Kwanza: Kulinda eneo linalojulikana au linaloshukiwa la kaburi au maeneo ya utupaji mwili, ICMP. ST.AA.857.1 www.icmp.int/wp-content/ uploads/2018/10/icmp-st-aa-857-1-docguidelines-for-first-response-at-grave-or-bodydisposal-locations.pdf • ICMP (2019), Kanuni za ICMP Paris, Toleo la Kiokezo, ICMP.DG.468.1.W.doc www.icmp.int/ wp-content/uploads/2019/04/icmp-dg-1468-1-Wdoc-paris-principles-annotated.pdf • Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) (2009), Kanuni za Kuongoza/Sheria ya Mfano kuhusu Kupotea www.icrc.org/en/document/ guiding-principles-model-law-missing-model-law

• ICRC (2016), Usimamizi wa Maiti Baada ya Majanga: Mwongozo wa Eneo la Kazi kwa Wahudumu wa Kwanza www.icrc.org/en/ publication/0880-management-dead-bodiesafter-disasters-field-manual-first-responders • ICRC (2020), Kuandamana na Familia za Watu Waliopotea - Mwongozo halisi https://shop.icrc. org/accompanying-the-families-of-missingpersons-a-practical-handbook-pdf-en • Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (2008), Kanuni za Maadili ya Wachunguzi, ICC/AI/2008/005 www.icc-cpi.int/resource-library/Vademecum/ Code%20of%20Conduct%20for%20Investigators. PDF • Interpol, (2018) Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga www.interpol.int/en/How-we-work/ Forensics/Disaster-Victim-Identification-DVI • Muungano baina ya Wabunge na ICRC (2009), Watu Waliokosa -Mwongozo wa Wabunge www.icrc.org/en/doc/assets/files/other/ icrc_002_1117.pdf • Kikundi cha Sheria na Sera za Umma za Kimataifa (PILPG) (2015), Mwongozo wa Eneo la Kazi kwa Uchunguzi wa Asasi za Kiraia na Kumbukumbu ya Ukiukaji Mkubwa wa Haki za Binadamu www.publicinternationallawandpolicygroup.org/ toolkits-and-handbooks • Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Upoteaji Unaotokana na Mamlaka, Kanuni za Kuongoza za kutafuta watu waliopotea (8 Mei 2019) Hati ya UN ya CED/C/7 www.ohchr.org/_ layouts/15/WopiFrame.aspx?sourcedoc=/ Documents/HRBodies/CED/CED_C_7_E_FINAL. docx&action=default&DefaultItemOpen=1 • Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (2004), Itifaki ya Istanbul - Mwongozo kuhusu Uchunguzi Madhubuti na Kumbukumbu ya Mateso na Matendo Mengine ya Ukatili, Matendo yasiyo ya Kibinadamu au ya Kudhalilisha au Adhabu www.ohchr.org/documents/publications/ training8rev1en.pdf • Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (2016), Itifaki ya Minnesota kuhusu Uchunguzi wa Vifo Vinavyowezekana Kuwa Haramu www.ohchr.org/Documents/Publications/ MinnesotaProtocol.pdf • Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (2001), Mwongozo wa Mafunzo kuhusu Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu www.ohchr.org/Documents/ Publications/training7Introen.pdf

17


Kiambatisho cha 2 Utaalamu unaofaa wa uchunguzi na uchunguzi wa kisheria unaweza kujumuisha wahusika au taaluma zifuatazo za wataalam: Msimamizi wa vifo vya halaiki anachukua jukumu la jumla kwa usimamizi wa uendeshaji shughuli katika makaburi ya halaiki ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, kuzingatia makubaliano ya mamlaka na Taratibu za Kawaida za Uendeshaji; kudumisha ushirikiano na jamii, afya, usalama na ustawi kwenye eneo; utekelezaji wa miundo ya kuripoti na mkakati wa mawasiliano; na uratibu wa utambulisho na mchakato wa urejeshwaji wa mabaki ya binadamu. Wachunguzi wa eneo la uhalifu/maafisa wakuu wa eneo ni watu waliofunzwa kutambua, kuweka kumbukumbu, kukusanya na kuhifadhi ushahidi halisi kwa uchambuzi zaidi wakati huo huo wakidumisha mfululizo wa kumbukumbu. Wataalamu wa data dijitali ili kuchunguza na kutoa ushahidi na data kutoka kwa simu za mkononi, kadi za hifadhi, kompyuta au mitandao ya jamii. Anthropolojia ya uchunguzi wa kisheria inahusika na urejeswahji na uchunguzi wa mabaki ya binadamu (ikiwa ni pamoja na yanayooza, mifupa, yaliyotengenishwa au kuchomeka) ili kujibu maswali ya sheria na kimatibabu, ikiwa ni pamoja na yale ya utambulisho. Akiolojia ya uchunguzi wa kisheria inaashiria utumiaji wa njia zilizotumika katika utafutaji wa mabaki ya zamani na vitu kwa madhumuni ya kisheria, ili kurekodi, kuchimba, kurejesha, kujenga upya na kutathmini eneo la uhalifu. Uchunguzi wa kisheria wa makombora/Wataalamu wa silaha na alama baada ya kutumia zana wanahusika katika uchunguzi wa alama zilizoachwa kwenye maonyesho na kulinganisha hizi pamoja

18

na vifaa/zana/silaha zinazowekana kusababisha, na kutoa hitimisho la thamani ya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na majeraha ya risasi na roketi zilizopatikana kutoka kwao. Entomolojia ya uchunguzi wa kisheria ni uchunguzi wa wadudu katika mazingira ya uchunguzi wa kisheria, mara nyingi kama sehemu ya patholojia ya uchunguzi wa kisheria, kama kiashiria cha wakati mdogo zaidi tangu kifo. Odontolojia ya uchunguzi wa kisheria ni uchunguzi wa meno kuhusiana na sheria, haswa katika uchunguzi wa kifo, haswa kwa utambulisho wa mabaki ya binadamu. Dawa za uchunguzi wa kisheria zinahusu kanuni na mazoea ya dawa kama zinavyotumika kwa mahitaji ya sheria na mahakama. Mwanapatholojia wa uchunguzi wa kisheria au daktari wa uchunguzi wa kisheria ni mtaalam aliyeidhinishwa wa matibabu ambaye ameidhinishwa kufanya uchunguzi wa kisheria wa baada ya kufa. Uchunguzi wa kisheria wa athari ya sumu ni sayansi ya dawa na sumu inayotumika kwa mahitaji ya kisheria na mahakama. Wataalamu wa utambulisho wa wanadamu wakiwemo wataalamu wa jeni, wataalam wa alama za vidole, wanabiolojia wa molekuli/wataalam wa uchunguzi wa kisheria wa DNA, au madaktari wa meno wa uchunguzi wa kisheria. (Chanzo: ilitolewa kutoka Itifaki za Minnesota, ukurasa wa 30 na 53)

Kila moja ya taaluma/wataalamu hawa watasimamiwa na kanuni husika na zinazofaa za za maadili. Vyeo vyao vinaweza kutofautiana.


Kiambatisho cha 3: Ugunduzi, kuripoti na ulinzi* Uthibitishaji na tathmini

Uchambuzi wa Data

Kuripoti kaburi

Simu

Zana na mbinu za upimaji wa ardhi

Picha

Ramani

Satelaiti

Ufikiaji wa eneo

Kuhisi mbali

Utambuzi wa kisheria

Ruhusa

Ushirikiano wa jamii

Muktadha wa eneo

Ulinzi wa mwili kutoka na

Mahali Usumbufu wa wanyama

Usumbufu Hatari

Ulinzi kupitia

Hali ya Hewa

Upeo wa Upitaji wa sehemu wakati ya ardhi Eneo Mamlaka

Video Ulinzi wa sehemu mlalo * Michakato iliyoonyeshwa katika Kiambatisho hiki ni sehemu muhimu ya ulinzi wa kaburi la halaiki na juhudi za uchunguzi.

Uzio

Ulinzi wa kisheria

Usalama 19


Kiambatisho cha 4: Mchakato wa uchunguzi* Awamu ya kupanga: 1

Awamu ya uchunguzi wa kisheria:

Ni huluki gani ina jukumu la jumla la juhudi za watu waliopotea?

1

Matumizi ya Taratibu za Kawaida za Utekelezaji

Nani anapaswa kupanga kuhusu uchunguzi wa kaburi la halaiki?

2

Ushughulikiaji wa ushahidi, mfumo wa kurekodi na kuhifadhi • Kurejesha • Usafirishaji • Kumbukumbu ya ushahidi • Kurekodi • Mfululizo wa kumbukumbu • Kuhifadhi

3

Mbinu za kudhibiti ubora

4

Muunganisho wa mkakati wa mawasiliano na timu ya mawasiliano

Je, upeo wa uchunguzi ni upi? Washirika wagani wa timu? Je, ni mamlaka gani za ziada zinazohusika na zinazohitajika? Ni shughuli gani zingine za uchunguzi?

2

Ufikiaji wa jamii na athari

3

Upeo, kiwango na mpangilio

4

Rasilimali, timu na ununuzi

5

Usalama na Ulinzi

6

Kutumia Taratibu za Kawaida za Uendeshaji

7

Sababu za nje na muktadha

8

Kushughulikia, kuhifadhi, kudumisha na kulinda data

9

Kurudishwa kwa mabaki ya binadamu na/au uhifadhi wa baada ya ufukuaji wa maiti

10

Mkakati wa mawasiliano 10.1

Ya ndani

10.2

Ya nje kati ya timu na mamlaka

10.3

Ya nje kati ya timu, familia, jamii na vyombo vya habari * Michakato iliyoonyeshwa katika Kiambatisho hiki ni sehemu muhimu ya ulinzi wa kaburi la halaiki na juhudi za uchunguzi.

20


Kiambatisho cha 5: Juhudi za utambuzi*

+ Ukusanyaji wa data na sampuli za DNA kutoka kwa familia: • Nyeti

• Kuheshimu haki za faragha

Mfumo wa usimamizi wa data • Usajili wa watu waliopotea • Maelezo kutoka kwa familia na Sampuli za DNA • Uchimbaji wa eneo na ushahidi • Matokeo ya chumba cha kuhifadhi maiti • Maabara ya DNA, wasifu na kulinganisha

Mawasiliano na uhamasishaji Mkakati wa mawasiliano: • Sahihi • Haijulikani • Kwa wakati unaofaa • Utiifu wa faragha na ulinzi wa data

Mawasiliano na: • Familia • Mamlaka • Vyombo vya habari

Mawasiliano kuhusu: • Mchakato wa utambulisho • Matokeo • Maendeleo • Muda uliowekwa • Usaidizi wa kisaikolojia

Mamlaka/afisa mchunguzi wa vifo anayetoa utambulisho au cheti cha ripoti ya kutokuwepo

• Udumishaji na uhifadhi unaoendelea

• Mazishi yanayofaa kitamaduni au kidini

• Michakato ya maabara • Hifadhidata ya wasifu wa DNA • Kulinganisha DNA

= Matokeo ya utambulisho

Kutenga jina/utambulisho sahihi kwa mabaki ya binadamu

Mwili uliotambuliwa lakini haujadaiwa na familia

Uwezo wa uchakataji wa DNA

Hakuna hitimisho kuhusu utambulisho

Kurudishwa kwa mabaki ya binadamu yaliyotambuliwa • Kutolewa kwa familia

• Mawasiliano kuhusu pendekezo la usaidizi

Katika hali ya kutotambuliwa • Udumishaji unaoendelea na ufuatiliaji (kuweka lebo, ramani, kuweka katika

kumbukumbu) ya mabaki ya binadamu • Cheti cha kutokuwepo

* Michakato iliyoonyeshwa katika Kiambatisho hiki ni sehemu muhimu ya ulinzi wa kaburi la halaiki na juhudi za uchunguzi.

21


Kiambatisho cha 6: Ukweli, haki na ukumbusho*

Utoaji wa maelezo

Kupokea maelezo

Kutoa maelezo

Uchunguzi

Ukumbusho

Maombolezo Maombolezo ya mtu binafsi ya pamoja

Utangazaji Rasmi Mazoea ya kidini

Mazoea ya kitamaduni

Haki ya jinai

Uhalifu

* Michakato iliyoonyeshwa katika Kiambatisho hiki ni sehemu muhimu ya ulinzi wa kaburi la halaiki na juhudi za uchunguzi.

22

Mashataka ya jinai

Suluhisho • Fidia • Marejesho • Urekebishaji • Kuridhika • Dhamana za kutorudia


Waandishi Dak. Melanie KLINKNER

Mkuu wa Masomo katika Sheria ya Kimataifa, Idara ya Binadamu na Sheria, Chuo Kikuu cha Bournemouth

Dak. Ellie SMITH

Mtafiti, Idara ya Binadamu na Sheria, Chuo Kikuu cha Bournemouth na Mshirika Mkuu wa Kampuni ya Usalama wa Ulimwenguni na Usimamizi wa Majanga

Washiriki-wataalamu wa mazungumzo ya ana kwa ana Esma ALICEHAJIC

Dak. Alessandra LA VACCARA

Sareta ASHRAPH

Dean MANNING

Mwanaakiolojia wa Uchunguzi wa Kisheria na Mwanaanthropolojia, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Wakili katika Baraza la Mahakama la Garden; Mkurugenzi, Ofisi ya Uchunguzi katika Eneo kwa Timu ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ili Kuhamasisha Uwajibikaji kuhusiana na Uhalifu Uliofanywa na Da’esh/ISIL;Mshauri Mkuu wa juhudi za uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa katika Syria na Iraq; Mwalimu Mgeni katika Shule ya Masomo ya Kiserikali ya Blavatnik, Chuo Kikuu cha Oxford

Caroline BARKER

Msimamizo wa Mpango wa Wahamiaji na Wakimbizi Waliopotea, Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea Mpelelezi wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika Yugoslavia ya zamani, mwanachama wa Timu ya Uchunguzi wa Pamoja ya MH17, na Kiongozi wa Timu ya Jopo la Kuchukua Mali ya Canberra

Peter MCCLOSKEY

Wakili Mwandamizi wa Kesi katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika Yugoslavia ya zamani (amestaafu)

Mwanaakiolojia wa Uchunguzi wa Kisheria na Mwanaanthropolojia, Mkuu wa Kitengo, Mwanaanthropolojia wa Uchunguzi wa Kisheria, Timu ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ili Kukuza Uwajibikaji kwa Uhalifu Uliofanywa na Da’esh/ISIL (UNITAD)

Bw. Howard MORRISON

Dak. Denis BIKESHA

Dak. Claire MOON

Mkuu wa Kitivo cha Shule ya Sheria, Chuo Kikuu cha Rwanda

Claudia BISSO

Mwanaanthropolojia wa Uchunguzi wa Kisheria, Timu ya Jopo la Watu Waliopotea wla Afrika Kusini na mshirika wa Timu ya Anthropolojia ya Uchunguzi wa Kisheria katika Ajentina (EAAF)

Dak. Agnes CALLAMARD

Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mauaji ya Kiholela, Yasiyo ya Haki au Yasiyo na Msingi

Tina GAENTZLE

Afisa Ujasusi wa Uhalifu wa Jinai, Usaidizi wa Upelelezi wa Wakimbizi/Uhalifu Mkubwa wa Kimataifa, INTERPOL

Alistair GRAHAM

Kiongozi wa Timu ya Uchunguzi, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai

Dak. Ian HANSON

Mwanaakiolojia na shahidi mtaalam wa uchunguzi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Akiolojia na Anthropolojia katika Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea; Mchunguzi katika Chuo cha Sayansi ya Uchunguzi wa Kisheria cha Marekani; Mchunguzi Mgeni katika Chuo Kikuu cha Bournemouth

Wakili wa Uingereza na Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hapo zamani, Baraza la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika Yugoslavia ya zamani Profesa Mshirika katika Idara ya Sosholojia, Shule ya Uchumi ya London na kiongozi wa utafiti kwa mradi wa ‘Haki za Binadamu, Mabaki ya Binadamu: Ubinadamu katika Uchunguzi wa Kisheria na Siasa za Kaburi’

Mark MUELDER

Mratibu wa kitengo cha Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga cha INTERPOL

Gauri PRADHAN

Kamishna wa zamani (Mwanachama) na Msemaji wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (NHRC), shirika la kitaifa la kikatiba la Nepali

Stefan SCHMITT

Kiongozi wa Mpango wa Uchunguzi wa Kisheria wa Kimataifa katika Kituo cha Kitaifa cha Sayansi na Teknolojia cha Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida, mwanachama wa Madaktari wa Haki za Binadamu na mwanzilishi wa Wakfu wa Anthropolojia ya Uchunguzi wa Kisheria wa Guatemala

Ali SIMOQY

Mtafiti huru, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanachama wa Timu ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ili Kukuza Uwajibikaji kwa Uhalifu Uliofanywa na Da’esh/ISIL (UNITAD)

Carolyn HORN

Dak. Deborah RUIZ VERDUZCO

Mshauri Mkuu na Mwandishi Maalum kuhusu Mauaji ya Kiholela, Yasiyo ya Haki au Yasiyo na Msingi

Mkuu wa Mipango ya Asasi za Kiraia, Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea

Andreas KLEISER

Rupert SKILBECK

Mkurugenzi wa Sera na Ushirikiano, Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali REDRESS, wakili na Mkurugenzi wa zamani wa Mashauri katika Mpango wa Haki wa Jumuiya ya Wazi

Wanachama wa Kikundi cha Uendeshaji Profesa Roger BROWNSWORD

Profesa Dinusha MENDIS

Profesa Louise MALLINDER

Dak. Annelen MICUS

Profesa wa Sheria katika Chuo cha Kings College London na Chuo Kikuu cha Bournemouth Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Queen’s Belfast

Profesa wa Mali ya Uvumbuzi na Naibu Mkuu wa Kitivo kwa Utafiti na Kazi ya Kitaalam katika Chuo Kikuu cha Bournemouth Mkuu wa Mpango wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya Bonavero katika Chuo Kikuu cha Oxford

Waandishi wanashukuru wataalam wengi walioshiriki katika awamu ya mashauri isiyofichua utambulisho na ambao maoni na mapendekezo yamekuwa muhimu sana kwa ukuzaji wa hati hii. 23




10856 09/20

Mradi huu unafadhiliwa na Baraza la Utafiti wa Sanaa na Binadamu la Uingereza. Sanaa na Binadamu huchunguza maadili na imani ambazo zinathibitisha sisi ni nani kama watu binafsi na jinsi tunavyotekeleza majukumu yetu kwa jamii yetu na kwa ubinadamu ulimwenguni.

26


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.